Saturday, 8 October 2022

BENKI YA DUNIA YAKOSHWA NA MIRADI YA MAJI INAYOTEKELEZWA NA RUWASA

...

 

Ukaguzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Ibubu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ukiendelea ambao umefadhiliwa na benki ya dunia.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

BENKI ya Dunia imetembelea na kuona utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ambayo imetoa fedha kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.
Ziara ya kutembelea miradi hiyo imefanyika leo Oktoba 8, 2022 kwa kukagua miradi ya maji katika kijiji cha Ibubu wilayani Shinyanga, na kijiji cha Banhi Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, ambayo inatekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA.

Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Rwegoshora Makaka, akizungumza kwenye ziara hiyo amepongeza miradi ya maji ambayo imetekelezwa na RUWASA, na kutoa wito kwa wananchi waitunze miundombinu ya miradi hiyo ya maji.

"Nawapongeza RUWASA kwa utekelezaji wa miradi hii ya maji, nawaomba tu wananchi muitunze miundombinu," amesema Makaka.

Aidha, ametoa ushauri kwa jumuiya za watumiaji maji, kukaa na kujadili kuona namna ya kuwasaidia wazee ambao hawajiwezi na hawana uwezo wa kununua maji,ili wawapatie huduma ya maji bure.

Nao baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo kwa nyakati tofauti, wameishukuru Benki ya Dunia, Pamoja na RUWASA, kwa kuwatekelezea miradi hiyo ya majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria, ambayo imewaondolea adha ya kutumia maji machafu pamoja na kupoteza muda wa shughuli za kiuchumi kwa kufuata maji umbali mrefu zaidi ya Kilomita 8.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Shinyanga Mhandisi Andrew Mogella, akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Ibubu, amesema utahudumia wananchi 2,554 na umegharimu Sh.milioni 454.3.

Meneja wa RUWASA wilayani Kahama Magili Maduhu, akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Banhi Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, amesema unahudumia wananchi 2,950 na umegharimu Sh.milioni 233.4.

Pia miradi mingine ambayo imekaguliwa ni ujenzi wa matundu ya choo 31 katika Shule ya Msingi Mahembe Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, ambayo yamegharimu Sh.milioni 39.1.

Mradi Mwingine ni ujenzi wa matundu ya choo Nane katika Zahanati ya Mwakata Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama yenye Thamani ya Sh.milioni 38.2 ambapo katika mradi huo ulionekana kuwa na dosari na kuagizwa ufanyiwe marekebisho.

Katika ziara pia ilikuwa na wataalum na wasimamizi wa miradi kutoka RUWASA Makao Makuu, Wizara ya Maji, Afya na Mazigira.
Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia nchini Tanzania Rwegoshora Makaka akizungumza kwenye ukaguzi wa miradi hiyo ambayo imefadhiliwa na benki ya dunia.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela akizungumza kwenye ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi ya maji ambayo imetokana na fedha za benki ya dunia.

Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga Mhandisi Andrew Mogella akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Ibubu wilayani Shinyanga.

Meneja wa RUWASA wilayani KAHAMA Mhandisi Maduhu Magili akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Banhi halmashauri ya Msalala.

Mzee Jigwese Njige mkazi wa kijiji cha Ibubu akitoa shukrani kwa kutekelezewa mradi wa maji safi na salama katika kijiji hicho.

Ukaguzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Ibubu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ukiendelea ambao umefadhiliwa na benki ya dunia.

Ukaguzi kituo cha kuchotea maji katika kijiji cha Ibubu ukiendelea.

Ukaguzi kituo cha kuchotea maji katika kijiji cha Ibubu ukiendelea.

Ukaguzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Banhi halmashauri Msalala ukiendelea ambao umefadhiliwa na benki ya dunia.

Usikilizaji wa taarifa ya mradi wa maji katika kijiji cha Banhi ukiendelea ambao umefadhiliwa na Benki ya dunia.

Awali ukaguzi wa matundu ya choo katika shule ya Msingi Mahembe Kata ya Mwakitolyo ukiendelea.

Ukaguzi wa matundu ya choo katika Zahanati ya Mwakata ukiendelea.
Ukaguzi ujenzi wa matundu ya choo katika Zahanati ya Mwakata ukiendelea.

Ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo itokanayo na fedha za benki ya dunia ikiendelea.

Ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo itokanayo na fedha za benki ya dunia ikiendelea.

Ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo itokanayo na fedha za benki ya dunia ikiendelea.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger