Thursday 24 February 2022

WATUMISHI SITA WAFUKUZWA KAZI HALMASHAURI YA SHINYANGA

...

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 23,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy. Wa Kwanza kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Christina Mzava akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Isaack Sengelema.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga limewafukuza kazi Watumishi Sita kutokana na makosa mbalimbali ya kiutumishi.

Uamuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 23,2022.

Mboje amesema Baraza la Madiwani limewafukuza watumishi hao baada ya kupitia utetezi wao na baadhi yao hawajaonekana kutokana na kutokuwepo kwenye maeneo yao ya kazi.

“Baraza la Madiwani limewafukuza kazi watumishi sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kutoka Idara ya Afya watumishi wawili wamefukuzwa kazi na kutoka Idara ya Utawala waliofukuzwa kazi ni wanne”,amesema Mboje.

Mbali na watumishi hao sita kufukuzwa kazi, pia watumishi wengine wawili Baraza hilo limeagiza wakatwe asilimia 15 ya mishahara yao na watafanya hivyo kwa muda wa miaka mitatu.

Watumishi Idara ya Afya waliofukuzwa kazi ni Daktari Fidelis Benedict Mushi wa Kituo cha afya Nindo na Andrew Israel Mwakisambwe ambaye ni Mteknolojia Maabara Kituo cha Afya Salawe.

Watumishi wanne kutoka Idara ya Utawala waliofukuzwa kazi ni Maafisa Watendaji wa Vijiji ambao Charles Dominick Mayunga (Bukene), Mercy Gasper Kyando (Kilimawe), Omary Hamis Omary (Igembya) na Robert Surika Mbuti (Mwabagehu).

Soma pia : 

HALMASHAURI YA SHINYANGA YAPOKEA SH. MILIONI 900 KUPANGA, KUPIMA NA KULIPA FIDIA VIWANJA



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger