Tuesday 8 February 2022

CHOO CHA SHULE CHAPOROMOKA ... CHAUA NA KUJERUHI WANAFUNZI

...


MWANAFUNZI mmoja alifariki na wengine watatu walilazwa hospitalini baada ya choo cha shule ya upili ya Nyabondo kuporomoka. Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi alasiri katika eneo la Nyakach, kaunti ya Kisumu nchini Kenya.

Wanafunzi watatu waliookolewa walikimbizwa katika hospitali ya misheni ya Nyabondo ambapo wanaendelea kupokea matibabu. Aliyekuwa CEC wa kaunti ya Kisumu Vincent Kodiera alisema kuwa choo hicho kiliporomoka kikiwa na wanafunzi wanne na kwa bahati mbaya mmoja wao akapoteza maisha.

Polisi walifika kwenye eneo la tukio na marehemu akatolewa kutoka alikokuwa amenaswa. Kodiera ambaye aliwapa pole shule na familia ya mwanafunzi aliyefariki alitoa wito wa amani katika taasisi hiyo na maombi.

Alisema kuwa sasa sio wakati wa kunyoosheana vidole vya lawama na kuongeza kuwa lazima mwili wa mwanafunzi huyo ungetolewa. “Tumeona maafisa wa polisi hapa na tunajua uchunguzi utafanywa kuhusiana na tukio hilo,” alisema.



Gavana wa Kisumu Anyang’ Nyong’o alituma risala zake za rambirambi kwa familia, walimu na wanafunzi wenza wa marehemu katika shule ya Upili ya Nyabondo. Nyong’o vilevile aliwatakia afueni ya haraka wanafunzi waliojeruhiwa katika ajali hiyo.


Gavana huyo alisema serikali ya kaunti ilituma vikosi vya waokoaji katika eneo la tukio ambao walijaribu kila wawezalo kumuokoa mvulana huyo anayesemekana kuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger