Friday 11 February 2022

SABABU KIFO CHA MWELE MALECELA

...

BAADA ya kusambaa kwa taarifa za kusikitisha kuhusu aliyekuwa Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele, Dk. Mwele Ntuli Malecela kufariki dunia, jana Alhamisi, Februari 10, 2022, Geneva mchini Uswisi, familia ya marehemu imetaja chanzo cha kifo hicho.

Kaka wa Marehemu William Malecela maarufu kama Lemutuz amesema kifo cha dada yake kimesababishwa na kansa.

“Ni kweli amefariki leo Hospitalini Geneva, Switzerland alikua anasumbuliwa na Kansa, msiba utakuwa Dodoma,” amesema Lemutuz.

Mwele Ntuli Malecela alizaliwa tarehe 26 Machi 1963, alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiafya Tanzania (NIMRI). Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.



Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela alikua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo alikua Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele.



Mwele Ntuli Malecela alizaliwa tarehe 26 Machi 1963, alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI). Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela alikua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo alikua Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger