Sunday, 27 February 2022

MAPIGANO MAKALI NA MILIPUKO YARIPOTIWA UKRAINE

...

Mji mkuu wa Ukraine, Kiev umekabiliwa na shambulio makali ya Urusi usiku wa kuamkia leo Februari 27, 2022. Wakati huo huo, mataifa ya Magharibi yanapanga kuiondoaUrusi kutoka kwenye mfumo wa fedha wa kimataifa (SWIFT).

Taarifa ya jeshi la Ukraine imesema kuwa wanajeshi hao wa Urusi pia wanakabiliwa na upinzani mkubwa ikiwa pamoja na vikosi hivyo vya Ukraine kuzuia shambulio la Urusi karibu na mji wa Kharkiv ulio kaskazini, mashariki mwa Ukraine.

Ofisi ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy imesema kumetokea mlipuko kwenye bomba la gesi, kusini mwa mji mkuu wa Kiev mapema Jumapili. Amri ya kutotoka nje imewekwa katika mji huo mkuu wa hadi kesho Jumatatu.

Balozi wa Ukraine nchini Ujerumani Andrij Melnyk ameelezea furaha yake kutokana na uamuzi wa Ujerumani wa kupeleka silaha nchini Ukraine. Balozi Andrij Melnyk ameliambia shirika la habari la Ujerumani (dpa) kuwa hatua hiyo ni ya kihistoria.
th

Sasa kuna ripoti za mapigano katika mitaa ya Kharkiv. Wanajeshi wa Urusi waliingia katika jiji hilo katika saa moja iliyopita, maafisa wa eneo hilo wanasema.

Picha za mitandao ya kijamii zinaonekana kuonyesha baadhi ya vitengo vya jeshi la Urusi katika jiji hilo. Pia kuna picha zinazoonyesha angalau magari mawili ya Kirusi "Tiger" yakiwaka moto katika jiji hilo.

BBC bado haijathibitisha picha hizi.

Maafisa wa Kharkiv asubuhi ya leo wamewaonya wenyeji kukaa katika makazi na kutoka mitaani.

Social embed from twitter

• Licha ya onyo jana usiku kwamba Kyiv ingeshambuliwa na makombora ya Urusi, mlipuko wa angani hauonekani kutokea.

• Milipuko hata hivyo ilisikika karibu na jiji na ghala la mafuta huko Vasylkiv kusini mwa mji mkuu lilipigwa na kuchomwa moto, kulingana na meya wa eneo hilo. Moto huo ulizusha hofu ya moshi wenye sumu na wakaazi walionywa kufunga madirisha na kusalia majumbani

•Mji wa kusini wa Nova Kakhovka umechukuliwa na wanajeshi wa Urusi, meya wa jiji hilo alisema asubuhi ya leo.

• Wakati huo huo, magari ya Urusi yameingia katika jiji la pili kwa ukubwa nchini Ukraine, Kharkiv, wanasema maafisa wa Ukraine. Mlipuko mkubwa pia ulisikika mapema katika mji huo, ambapo bomba la gesi linasemekana kugongwa

• Maeneo ya makazi huko Kharkiv pia yalishambuliwa, kulingana na huduma za dharura. Mwanamke mmoja aliripotiwa kuuawa na makumi kadhaa kuhamishwa kutoka kwa jengo la orofa tisa

• Takriban vifo sita vya raia pia viliripotiwa katika mji wa Okhtyrka, kaskazini-mashariki mwa Ukraine, kulingana na meya wa eneo hilo.

• Katika saa iliyopita Idhaa ya BBC ya Kiukreni iliripoti akaunti mpya za milipuko huko Kharkiv na Kherson kusini-mashariki.

• Katika hatua ya kuiadhibu Urusi, Umoja wa Ulaya, Marekani na washirika wao watakata benki kadhaa za Urusi kutoka kwa mfumo mkuu wa malipo wa kimataifa, Swift. Pia watafungia mali ya benki kuu ya Urusi

• Australia imekuwa nchi ya hivi punde zaidi kutangaza kuwa itafadhili usambazaji wa silaha hatari kwa Ukraine ili kuisaidia kupambana na Urusi. Hatua hiyo imekuja baada ya Ujerumani kuamua Jumamosi kusambaza silaha kwa Ukraine, ikiwakilisha mabadiliko makubwa ya sera

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger