Naibu Waziri Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe. Geofrey Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla alipotembelea viwanda vya kuchakata mazao katika vilivyopo katika kata ya Maji Moto Mkoani Katavi.
Naibu Waziri Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe. Geofrey Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla wakionyesha mchele unaozalishwa na moja ya kiwanda Kinachopatika katika eneo la Maji Moto Mkoani Katavi.
Naibu Waziri Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kavuu Mkoani Katavi Mhe. Geofrey Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni cha Wageni mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha Flamingo Foods Company Limited kujionea ukarabati mkubwa uliofanyika katika kiwanda hicho baada ya maghala ya kuhifandhia mchele kuezuliwa na upepo mkali uliotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Katavi.
Naibu Waziri Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe. Geofrey Mizengo Pinda (kushoto)akiangalia namna mtanbo wa kukamlia mafuta ya alizeti unavyofanya kazi. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla.
..............................................................
Na. Dennis Buyekwa- Katavi.
Wafanya biashara Mkoani Katavi wametakiwa kukata bima kwa ajili ya kulinda biashara zao wakati wanapokabiliwa na majanga mbalimbali yanayotokana na moto, mafuriko pamoja na upepo hatua itakayosaidia kuepuka gharama pale watakapohitaji kuendelea na uzalishaji baada ya majanga hayo kutokea.
Hayo yamezungumzwa mapema leo na Naibu Waziri, Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Geofrey Mizengo Pinda alipowatembelea wafanyabiasha wanaomiliki viwanda vya kuchakata Mchele, Karanga na alizeti ili kijionea ukarabati wa majengo ya kuhifadhia bidhaa yaliyoezuliwa na upepo mkali uliotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika eneo la Maji moto lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi.
Akiwaelezea faida watakazo pata wafanyabiashara hao kwa kukatia bima biashara zao Mhe. Pinda amesema kuwa faida kubwa watakayoipata wafanya biashara hao ni kutosimamisha huduma zao kwa muda mrefu kwa kuwa pindi majanga yatakapotokea kampuni husika zitawalipa fidia na hivyo kuwafanya waendelee kuwahudumia wananchi wao bila kikwazo chochote.
Mhe. Pinda ameendelea kueleza kuwa iwapo wamiliki wa viwanda hivyo watafanikiwa kukata bima kwa ajili ya miradi hiyo itawasaidia kuendesha shughuli zao pasipo na shida yoyote hatua itakayoisaidia Serikali pia kuendelea kupata mapato wakati wote kwa sababu sasa watakuwa na uhakika na huduma wanazotoa kwa wananchi na hivyo kuendelea kuchangia ukuaji wa pato la Taifa.
“nawahimiza kukata bima, kwa sababu ukiwa na bima kwenye mradi wako unakuwa hauna cha kuhofia wakati wa kuendesha shughuli zako hata likitokea la kutokea kampuni za bima zitakulipa ndani ya muda mfupi, hatua itakayosaidia kuendelea na uzalishaji bila wasiwasi. Alisema Mhe. Pinda.
Ameongeza kuwa bima hizo pia zitawasaidia wafanya biashara kuwa na soko la uhakika kwa kuwa sasa wateja wao watakuwa na uhakikika wa kupata huduma zao kwa ufasaha kwa kuwa sasa wafanyabiashara hao watawezakuongeza uzalishaji wa bidhaa na ajira kwa ujumla nchini kwa vile hata majanga yakitokea uzalishaji hautasimama kwa muda mrefu.
Aidha, Mhe. Pinda ametoa wito kwa wamiliki wa bidhaa hizo kuhakikisha wanapata vifungashio vya kisasa kwa ajili ya kufungasha bidhaa zao kwani kwa kufanya hivi itawasaidia kuongeza thamani ya bidhaa zao, kuongeza wigo wa kuamiwa na wateja kujitangaza wao wenyewe pamoja na mkoa wa Katavi kwa ujumla.
“tunataka ulimwengu ujue Maji Moto kuna mchele, karanga na alizeti ili kila atakayetumia bidhaa mnazozalisha ajue kuwa bidhaa hizi zinapatikana Majimoto hapa Katavi”. Alisema Mhe. Pinda.
Akiwa viwandani hapo Mhe. Pinda alipata fursa ya kutembelea na kujione jinsi viwanda vivyo vinavyofanya kazi huku akiahidi kushughulokia changamoto zinazowakabiri wafanyabiashara hao ikiwemo tatizo la umeme ambao umekuwa ukikatika mara kwa mara na kupelekea kukwamisha uzalishaji mkoani humo.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Flamingo Foods Ndg. Leonard Lusaganya, amemshukuru Kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa eneo hilo kwa kufika kujionea halihalisi iliyopo katika viwanda vivyo huku akisema kuwa ziara hiyo imewaongezea ari ya kuendelea kuzalisha bidhaa nyingi na bora Zaidi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaongeza uzalishaji hatua itakayosaidia kupunguza tatizo la upatikanaji wa bidhaa hizo nchini.
Ndg. Lusaganya aliishukuru Serikali ya mkoa wa Katavi kwa kuboreshea mazingira mazuri ya uwekezaji ambapo imewasaidia kuongeza uzalishaji kwa kiwango kikubwa na hivyo kupelekea kuzalisha bidhaa zinazotosheleza mahitaji ya wananchi mpaka kufikia kufanya biashara ndani na nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment