Wednesday, 25 March 2020

Tanzania Yapokea Msaada Wa Vifaa Tiba Vya Corona Toka Kwa Mfanyabiashara wa China Jack Ma

...
Vifaa tiba vilivyotolewa na mfanyabiashara kutoka China, JackMa kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona nchini Tanzania vimewasili usiku wa kuamkia leo Machi 25, 2020, na ndege ya shirika la Ethiopia.

Katika taarifa yake aliyoiandika kupitia ukurasa wake wa  Twitter Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, amemshukuru mfanyabiashara huyo pamoja na Serikali ya China kwa ujumla.

"Jana usiku sisi Tanzania tulipokea mchango wa vifaa tiba, ambavyo vitasaidia katika mapambano yetu dhidi ya COVID-19, shukrani zetu za dhati kwa mfanyabiashara JackMa na taasisi yake ya AlibabaGroup na Serikali ya Ethiopia" Ameandika Waziri Ummy.

Vifaa hivyo ni barakoa 100,000, vipimo 20,000, na mavazi ya kujilinda (protective suits) 1,000.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger