Saturday, 28 March 2020

Kenya yaanza kutekeleza amri ya kutotoka nje wakati wa usiku ili Kukabiliana na Corona

...
Amri ya kutotoka nje nchini Kenya kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri ilianza kutekelezwa majira ya saa moja jana huku wafanyakazi wa huduma muhimu pekee wakiruhusiwa kuwa nje usiku.

Jana majira ya saa kumi na mbili Wakenya wengi mjini Nairobi walionekana wakiharakisha kuelekea nyumbani hatua iliyosababisha msongamano mkubwa katika barabara kadhaa huku wale waliokuwa wakitumia usafiri wa umma wakionekana kusubiri katika vituo vya magari hayo licha ya muda kuyoyoma.

Magari machache ya abiria mashuhuri kwa jina la ‘Matatu’ nchini Kenya yaliyokuwepo yalitumia fursa hiyo kujitengezea fedha baada ya kuongeza nauli huku baadhi yao yakikiuka agizo jipya la kupunguza idadi ya abiria ndani ya magari hayo ili kuwaepusha maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya Hillary Mutyambai alionya jana kwamba wale watakaopatikana nje ya nyumba zao baada ya saa moja usiku watakabiliwa iwezekanavyo.

Hata hivyo mjini Mombasa na Eldoret mpango huo ulianza kwa mkosi baada ya maafisa wa polisi kukabiliana na wakaazi saa mbili kabla ya amri hiyo kuanza kutekelezwa.


Credit:Parstoday



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger