Thursday 26 March 2020

MBOWE AJIWEKA KARANTINI BAADA YA MTOTO WAKE KUTHIBITIKA KUWA NA CORONA

...

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amejiweka karantini siku chache baada ya kutangaza kuwa mwanaye Dudley amepata maambukizi ya Corona.

Mbowe amesema amejitenga na familia yake ambayo itakuwa karantini kwa wiki mbili, na hivi sasa yupo nyumbani Dodoma akisubiri majibu ya vipimo ili kufahamu kama naye ana Virusi hivyo.

Akiongea na Clouds Media Mbowe amesema tangu aonane na Dudley siku 12 zilizopita, amekutana na watu wengi hivyo ni jambo la kuomba Mungu asikutwe na Corona ili aliokutana nao pia wawe salama.

Aidha, Mbowe ameeleza kuwa mkakati wa pamoja unahitajika ili kukabiliana na mlipuko wa Corona ambao amesema ni suala ya kitaifa.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger