Saturday 28 March 2020

WANAKIJIJI 6 WANUSURIKA KUFA KWA KUSHAMBULIWA NA FISI WALIYEMZINGIRA WAMUUE SHINYANGA

...
Picha haihusiani na habari hapa chini
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Watu sita wamenusurika kufa kwa kushambuliwa na fisi baada ya kumzingira wakitaka kumuua katika kijiji cha katika kijiji cha Mwangh’alanga, kata na tarafa ya Samuye, wilaya na mkoa wa Shinyanga. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Ijumaa Machi 27,2020 majira ya saa nne. 

“Chanzo cha tukio hilo ni watu hao kuvamiwa na fisi huyo baada ya kumzingira wakitaka kumuua. Hata hivyo wananchi walifanikiwa kumuua fisi huyo”,amesema Kamanda Magiligimba. 

Amewataja waliojeruhiwa kujeruhiwa na fisi kwa kung'atwa maeneo mbalimbali ya miili yao katika tukio hilo kuwa ni Zengo Jitonja , Nkuba Deteba , Juma Salaganda, Limbu Mihambo , Dutu Mdese na John Matana wote wakazi wa kijiji cha Mwangh’alanga Samuye 

Amesema majeruhi watano kati yao wamepata majeraha madogo madogo na hivyo wamepatiwa matibabu hospitalini na kuruhusiwa na hali zao zinaendelea vizuri. 

“Majeruhi mmoja Zengo Jitonja (56), amelazwa katika hospitali ya rufaa mkoa Shinyanga baada ya kujeruhiwa na fisi huyo mikononi na mdomoni na hali yake siyo mbaya sana”,ameongeza Kamanda Magiligimba.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger