Sunday 29 March 2020

JIKO LA MKAA LAUA WATU WANNE WA FAMILIA WAKIJIKINGA NA BARIDI YA MVUA SHINYANGA

...


Nyumba ambayo marehemu walikuwa wamelala

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia baada ya kuvuta ya hewa yenye sumu ya Carbon monoxide iliyotokana na mkaa waliowasha kwenye jiko la mkaa kisha kulala ndani ya nyumba yao wakijikinga na baridi katika kitongoji cha Ngilimba ‘B’ kijiji cha Ngilimba kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga. 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Machi 28,2020 ambapo ndugu hao wa familia moja waligundulika kuwa wamefariki dunia wakiwa nyumbani kwao wamelala baada ya kuvuta hewa yenye sumu ya Carbon Monoxide. 

“Chanzo cha tukio hilo ni kwamba siku hiyo mvua kubwa ilinyesha kijijini hapo na kupelekea uwepo wa baridi nyumbani kwa marehemu hao na ndipo wakati wakijiandaa kulala waliacha jiko la mkaa likiwa limewashwa ndani ya nyumba na kufunga mlango na dirisha hali iliyo pelekea mgandamizo wa hewa kuwa mdogo ndani ya nyumba yao na kuvuta hewa hiyo iliyokuwa na sumu ya carbon monoxide”,amesema Kamanda Magiligimba. 

“Waliofariki dunia ni Masanja Emmanuel (35), Mngole Masanja (25), Holo Masanja,(05) na Matama Masanja wote wakazi waNgilimba wote wa familia moja”,ameeleza Kamanda Magiligimba 

Amesema miili ya marehemu imekabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger