Tuesday 31 March 2020

Rais wa Uganda Yoweri Museveni atangaza amri ya kutotoka nje kwa siku 14 ili Kukabiliana na Corona

...
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametagaza masharti zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona wiki mbili baada ya kupiga marufuku usafiri wa Umma.

Katika hotuba yake kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni usiku wa Jumatatu ,Museveni amepiga marufuku usafiri wa kutumia magari binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku.

Mtu yeyote anayehitaji huduma za dharura za kiafya kama vile kujifungua au kufanyiwa upasuaji anatakiwa kupata idhini kutoka kwa maafisa wa serikali katika ngazi ya Wilaya kabla ya kutoka nyumbani

Wauzaji bidhaa za chakula sokoni watahitajika kuondoka maeneo yao ya biashara hadi pale serikali itakapokamilisha kushughulikia maeneo mapya ya wao kuuzia bidhaa zao .

Rais Museveni pia ameahidi msaada wa chakula kwa watu ambao hawafanyi kazi kutokana na vikwazo vya kukabiliana na covid-19 na hawana uwezo wa kujipatia bidhaa hiyo muhimu.

Museveni pia ametoa agizo kwa polisi kuwakamata wanasiasa watakaotoa misaada ya chakula kwa jamii na kushtakiwa kwa ''jaribio la mauaji ''

Uganda kufikia sasa imethibitisha kuwa na wagonjwa 33 wa corona na maafisa wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.

Magari binafsi yatazuiwa kuingia barabarani baada ya maelekezo ya awali kutaka magari kubeba abiria watatu pekee kukiukwa, na baadhi ya watu kutumia magari binafsi kuwasafirisha wengine na kuongeza hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo. 

-BBC


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger