Tuesday, 3 March 2020

Godbless Lema Akamatwa, Apelekwa Singida akituhumiwa kutoa taarifa za Uongo

...
Jeshi la Polisi mkoani Singida, limethibitisha kumkamata Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwa ajili ya mahojiano akituhumiwa kutoa taarifa zisizo sahihi zenye lengo la kulichonganisha jeshi hilo na wananchi mnamo Februari 29, 2020, wilayani Manyoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amesema mtuhumiwa Lema amekamatwa jana jioni mjini Arusha na kisha kusafirishwa hadi Singida mjini.

Amesema hivi karibuni Lema alipokwenda Manyoni kuhudhuria mazishi ya dereva wa boda boda Alex Joas alitumia fursa hiyo kupotosha wananchi kwamba  Jeshi la Polisi halikuchukua hatua zozote dhidi ya matukio ya mauaji ya wakazi 14 Wilaya ya Manyoni. 


Njewike amesema Lema atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger