Sunday, 3 November 2019

Wanawake wa jamii ya kibarbeig Babati kunufaika na utalii

...
Wanawake jamii ya Kibarbeig wilayani Babati, mkoa wa Manyara wanatarajiwa kuanza kunufaika zaidi na Utalii baada ya kuanzishwa vituo vya kuvutia watalii katika maeneo yao.

Afisa Maendeleo ya jamii ya Taasisi ya Chemchem association, Walter Palangyo amesema,Taasisi hiyo iliyowekeza shughuli za Utalii,katika hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge, kupitia hoteli za Kitalii za Chemchem imejipanga kuboresha maisha ya jamii hiyo ili inufaike zaidi na Utalii.

Ofisa Utamaduni wa wilaya ya Babati, Beatrice Maliseli  akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho Leo Jumapili Novemba 3, 2019, aliwataka wanawake wa jamii hiyo kukitumia  vizuri kujiongezea kipato.

Amesema sasa watalii wataweza kuwatembelea na kununua vifaa vyao , kuona ngoma na tamaduni zao na hivyo kujiongezea fedha kwa ajili ya maisha yao.

Maliseli aliwataka wanawake na vijana wa jamii hiyo,kuongeza ubunifu wa vifaa vyao na kuanza kujifunza lugha za kigeni ili waweze kuwasiliana vizuri na watalii.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger