Wednesday 27 November 2019

Naibu Waziri Masauni Aagiza Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar Aondolewe na Ashushwe Cheo

...
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro kufanya mabadiliko ya uongozi kwenye Chuo cha Polisi Dar es Salaam kutokana na kukiuka maagizo yake katika ujenzi wa mabweni chuoni hapo.

Pia, Masauni amemuelekeza IGP Sirro kumuondoa Mkuu wa Chuo hicho, Antony  Ruttashuburugukwa na kumshusha cheo kutokana na kosa hilo.

Akizungumza leo Jumatano Novemba 27, 2019 akiwa chuoni hapo, Masauni amesema alielekeza katika ujenzi huo watumike wafungwa kufanya kazi za vibarua ili kuokoa fedha lakini mkuu huyo wa chuo hakutekeleza agizo hilo.

“Rais alikubali kutupatia Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, tuliangalia na kuona tunaweza kuokoa Sh210 milioni za kuwalipa vibarua kwa kuwatumia wafungwa.”

“Nilizungumza na kamishna wa magereza akasema hilo linawezekana hivyo nikamuelekeza mkuu wa chuo kufanyia kazi suala hilo lakini leo nimekuja nakuta hali hii hakuna wafungwa,” amesema Masauni

Wakati Masauni anakagua ujenzi huo alikuta vijana wakifanya kazi na alipowahoji walimuleza kuwa wao ni vibarua wanaolipwa kwa siku.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger