Saturday 30 November 2019

Simbachawene: Matumizi Ya Nishati Mbadala Ni Kitu Cha Muhimu Kwa Maendeleo Ya Taifa

...
Matumizi ya nishati ya kuaminika na endelevu ni kitu kisichoepukika kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na kwa Taifa lolote duniani hasa tunapoelekea kufikia lengo la Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025. Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene alipokua akizindua maonyesho ya  14 ya kitaifa ya nishati jadidifu yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja , jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo  ni kuhakikisha kuwa masuala yote yanayokwamisha upatikanaji rahisi, ueneaji na ongezeko la matumizi ya Nishati hizi kwa wananchi wote hasa walioko vijijini na hata mijini linashughulikiwa ipasavyo.  ”Ninawashauri muwe tayari kupeleka huduma zenu vijijini kwa kuanzisha matawi ya biashara zenu huko badala ya kunga’ng’ania mijini pekee” alisema Waziri Simbachawene.

Aidha alisititiza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inathamini juhudi  za uendelezaji na uhamasishaji wa matumizi ya Nishati jadidifu na udhibiti wa ubora wa vifaa na ufungaji wa mitambo mbalimbali, ili kuwa na Teknolojia endelevu katika ustawi wa Mazingira yetu. Pia amewaagiza TAREA kufanya utafiti kubaini kwa kiasi gani jamii ya Wananchi katika mkoa wa Dar es Salaam wanatumia nishati jadidifu.

“Naye Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Bwana Jeroen Verheul amemshukuru Waziri Simbachawene lakin pia amesema kuwa wataendelea kufadhili masuala mbalimbali  ya mazingira yakiwemo yanayohusu nishati mbadala kama ambavyo wamefanya kwa TAREA.

Akiongea katika ufungzi huo Katibu wa Jumuia ya Nishati jadidifu Makamu Mwenyekiti wa TARE Bwana Prosper Magali, alimshukuru Waziri Simbachawene kwa kufungua maonyesho hayo na aliongeza kuwa TAREA itaendelea kushughulika na  masuala ya nishati jadidifu lakini pia wanachukua maelekezo ya Waziri aliyowapa na kuyafanyia kazi.

Maonyesho hayo ya nishati jadidifu yameandaliwa na Jumuia ya nishati jadidifu (TAREA) ambapo hufanyika kila mwaka. Kwa mwaka huu maonyesho hayo ymefanyika katika viwanja vya mnazi mmoja na mgeni Rasmi akiwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger