Wednesday 27 November 2019

RAIS MAGUFULI : ......KUSUSIA UCHAGUZI NAYO NI DEMOKRASIA

...
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kitendo cha kususia uchaguzi na kujitoa katika uchaguzi pia ni demokrasia huku akikisitiza kuwa maendeleo hayana chama na kwamba Watanzania wanatakiwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa. 

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatano Novemba 27,2019 wakati akizungumza na wananchi wa Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 

Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kukipongeza Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 24,2019 ambapo baadhi ya Vyama vya Upinzani nchini Tanzania vilisusia uchaguzi huo 

“Ninapenda kuwashukuru sana ndugu zangu wa Isaka mmemaliza chaguzi, Nimeambiwa Chama Cha Mapinduzi kimepasua vizuri. Hongereni sana,maendeleo ndugu zangu hayana chama na demokrasia hata kujitoa nayo ni demokrasia,kususia uchaguzi nayo ni demokrasia”,amesema Rais Magufuli. 

“Kwa hiyo nawapongeza kwa ushindi mkubwa mlioupata chama cha mapinduzi lakini maendeleo hayana chama ni lazima tushikamane wote kujenga taifa letu,tunachohitaji ni maendeleo,ukileta maji,wote watakunywa,uwe CCM, uwe CHADEMA,ukileta bandari hapa kila mmoja atafanya biashara”,ameongeza Rais Magufuli. 

“Naomba Watanzania tutangulize mbele maslahi ya taifa letu,tuwe wamoja,tujenge Tanzania yetu”,amesema Rais Magufuli.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger