Tuesday, 12 November 2019

RAIS MAGUFULI : “NILINYWESHWA SUMU DODOMA ALMANUSURA IONDOE UHAI WANGU”

...
Rais John Magufuli amesema utendaji wake wa kazi ulisababisha anyweshwe sumu na ilibaki kidogo apoteze maisha.

Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumanne Novemba 12, 2019 katika uzinduzi wa kitabu cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa cha Maisha Yangu, Kusudio Langu.

“Nakumbuka mzee Mkapa pale tulipofanya kazi vizuri alipata furaha hasa katika ujenzi wa barabara na baadaye akatamka kuwa mimi (Magufuli) ni askari wa mwamvuli namba moja.”

“Siwezi kusahau suala hilo maishani mwangu kwa kuwa liliniletea matatizo nilianza kuona dalili za baadhi ya mawaziri tena wengine wa ngazi za juu kuanza kunichukia,” amesema Magufuli.

Amebainisha kuwa baadaye alinyweshwa sumu, “nilinyweshwa sumu Dodoma almanusura iondoe uhai wangu lakini kwa neema za Mungu nikakiepuka kifo.”

“Baada ya kunusurika na kifo nilimfuata mzee Mkapa kumweleza dhamira yangu ya kutaka kujizulu. Nakumbuka siku hiyo aliniangalia jicho la baba na mwana akanihurumia, alinipa ujasiri akaniambia John kafanye kazi kamtangulize Mungu.”
CHANZO - MWANANCHI
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger