













Na Dixon Busagaga ,Moshi
WAFANYAKAZI wa Malmala ya Majisafi na Usafi wa MAzingira ,Moshi,(MUWSA) wamemuomba Waziri wa Maji ,Prof Makame Mbarawa kusaidia mchakato wa kufuatilia fedha za malimbikizo ya madeni ya maji kwa taasisi za serikali ambazo ni zaidi ya Sh Bil 2.3.
Mamlaka ya Majisafi an Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) ni miongoni mwa mamlaka zinazotajwa kufanya vizuri katika utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi inaowahudumia ambapo kwa sasa imefikia wastani wa asilimia 91% kwa eneo inayohudumia.
Licha ya mafanikio hayo yanayoitamburisha MUWSA kuwa miongoni mwa Mamlaka Bora nchini ,changamoto iko kwenye Madeni yatokanayo na Ankara za maji kutoka kwa taasisi za serikali .
Akizungumza wakati wa kuzindua bodi hiyo Waziri wa Maji, Prof.Mbarawa amesema Wizara kwa sasa imelekeza nguvu zake kwenye kusimamia makusanyo katika Mamlaka za Maji nchini ili kuweza kufikisha huduma ya maji katika maeneo mengi zaidi.
Katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ,Moshi (MUWSA) Waziri Mbarawa alisema ‘Wakati wangu wote natumia nguvu nyingi kusimamia makusanyo kwenye mamlaka za maji, ziko ambazo zikitaka hata kufunga nati kwenye miradi zinakuja wizarani kuomba fedha”alisema Prof Mbarawa.
Zaidi Mbarawa aliongeza: “Mamlaka hizi kama tutazisimamia vizuri zina uwezo mkubwa sana, lakini bado tuko kwenye usingizi. Nataka kila bodi mpaka watendaji wabadilike na kuiga mfano wa Mamlaka ya Maji ya Moshi Mjini”alisema .
“Mimi baada ya kuingia katika Wizara hii niliamua kuzifuatilia mamlaka kama saba ambayo ni Dar es Salaam, Moshi, Arusha, Morogoro, Mbeya na mamlaka za maji ndogo ndogo za Kilwa na Makonde.”
Alisema kasi ya ukusanyaji wa mapato kwa Muwsa, inampa moyo wa kuendelea kukaa katika Wizara hiyo hasa kutokana na takwimu kuonyesha kuna jitihada za kuongeza makusanyo yake kila mwezi.
“Mimi ukiniuliza, nasema Muwsa ina uwezo wa kukusanya Sh. bilioni 1.2 kwa mwezi na hilo halina ubishi, kwa sababu mwezi Januari 2019 tulikuwa tumekafika Sh. milioni 814,”alieleza Mbarawa
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Aron Joseph amesema hali ya utoaji wa huduma ya maji kwa sasa inaridhisha, kutokana na kutoa huduma katika kata 21 zilizopo ndani ya Manispaa ya Moshi na Wilaya ya Hai na Moshi Vijijini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza kabla ya Waziri Mbarawa kuhutubia, alisema kulikuwa na utitiri wa mamlaka za maji 159 nchi nzima lakini mamlaka hizo zimepungua sasa na kufikia mamlaka 83.
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Muwsa aliyemaliza muda wake, Prof. Faustine Bee ambaye kwa sasa ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alimweleza Waziri Mbarawa kuwa mpaka wanaondoka katika nafasi hiyo, deni la ankara za maji katika taasisi za umma ni Sh. bilioni 2.16
Pia, alimweleza kuwa mkakati mahususi waliouacha mchakato wake uendelezwe na bodi mpya ni pamoja na upanuzi wa mabwawa ya majitaka yanayopokea majitaka kutoka maeneo mbalimbali ambao gharama zake zinafikia Sh. bilioni 7.6
0 comments:
Post a Comment