Zaidi ya sh milioni 600 Za kitanzania zimetengwa na Halmashauli ya wilaya ya Ngara ili kujenga upya kituo cha afya Lukole kilichokuwa kimejengwa kwa tope na kilichokuwa kikiwahudumia wakimbizi waliokuwa wakiishi katika kambi hiyo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wakimbizi kutoka nchi jirani za Burundi na Rwanda waliokuwa wakiishi kambini hapo kuondoka na kituo cha afya kuendelea kuwahudumia wananchi wanaoishi jirani na kambi hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauli ya Ngara Aidan Bahama amesema kwa bahati mbaya kituo hicho kilijengwa kwa tope na kupelekea baadhi ya majengo Kuwa na hali mbaya na kuwa katika hatari ya kuanguka.
Kadhalika Aidan ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo na amemshukuru mh rais John Pombe Magufuli kwa kutoa pesa ambapo baada ya ujenzi huo kituo hicho kitakuwa ni moja ya vituo bora wilayani Ngara.
Nao baadhi ya wananchi na wafanyakazi katika kituo hicho cha Afya Ambao ni Bw Joseph Hezzron,bw James Charles,Bi Noral Charles Mihayo wameipongeza hatua hiyo ya serikali nakusema kuwa nijitihada za kujali huduma za wananchi.
Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa Jumla ya majengo sita yatajengwa katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na jengo la wagonjwa wa nje,jengo la upasuaji,maabara,jengo la kuhifadia maiti na nyumba moja ya mtumishi.
0 comments:
Post a Comment