Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Silent Ocean ,Salaa Mohamed amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika duka jipya na la aina yake la GSM Home ili kujipatia samani (fenicha) bora kabisa za kiwango cha kimataifa zinazoendana na kipato chao.
Mkurugenzi huyo aliyasema hayo Novemba 22, mwaka huu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa dMgeni rasmi katika Uzinduzi wa Duka jipya la GSM HOME lililopo Mikocheni A Barabara ya Mwai Kibaki jijini, na kuhudhuriwa na viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya GSM pamoja na wadau wengineo.
"Kwa mantiki hii, napenda niwapongeze kwa ajili ya kuendelea kuwa wabunifu na kuja na wazo la kuanzisha duka hili kubwa la samani ambalo linasaidia watu pamoja na taasisi kupata samani zenye ubora hapa nchini",alisema.
“Napenda kuwahimiza Watanzania kufika katika duka hili jipya na la aina yake ili kuweza kujipatia samani bora na ambazo zitaendana na kipato chao. Napenda niwapongeze GSM kwa kuendelea kuwa wabunifu na kuja na wazo la kuanzisha duka hili kubwa la samani ambalo linasaidia watu pamoja na taasisi kupata samani zenye ubora hapa nchini,” alisema Mohamed.
Alisema kutokana na uwepo wa makampuni ya GSM, maelfu ya Watanzania wameweza kupata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na hivyo kujipatia kipato kinachowasaidia kuendesha maisha yao.
“Makampuni ya GSM yamekuwa mdau muhimu na mwenye mchango mkubwa kwa nchi yetu na pia tunatarajia mchango wenu kuongezeka zaidi hasa katika utekelezaji wa lengo la kitaifa la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda pamoja na uchumi wa kati kufikia mwaka 2025,” alisema.
Aliongeza: “Napenda kuwahakishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, itaendelea kutengeneza mazingira mazuri na rafiki ya ufanyaji biashara ili kampuni kama GSM ziendelee kukua. Serikali imedhamiria kutekeleza mapendekezo yaliyopo kwenye waraka wa Blueprint yanayolenga kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini ili nchi yetu iweze kufika kwenye uchumi wa kati.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa GSM Group, Fatma Abdallah, lengo la kuzindua duka hilo ni kuziba pengo lililopo sokoni katika usambazaji wa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, lakini pia kuwasogezea wananchi huduma zao.
“Duka hili jipya linatarajiwa kuhudumia na kukata kiu kwa watanzania wote kwani mahitaji haya ni muhimu sana katika jamii yetu, hususan fenicha za majumbani na maofisini zinazopatikana hapa GSM HOME kwa ubora wa kimataifa.
Alizitaja bidhaa zinazopatikana katika duka lao hilo kuwa ni ‘shelving’, sofa, kabati za ukutani, meza za kahawa, meza za chakula, vitanda na fenicha za chumba cha kulala, makabati ya nguo na nyinginezo za kupendezesha ofisi na nyumba.
“Napenda kuwahabarisha Watanzania kuwa fenicha zetu ni bora na za kisasa zikiwa zimetengenezwa kwa umakini wa hali ya juu na kufanyiwa tathmini ya kubaini ubora wake wa kimataifa,” alisema.
Alisema mbali ya fenicha, wanauza vyombo vya aina zote vya jikoni, bafuni na chooni vya chapa (brand) kutoka Italia pamoja na vifaa vya umeme.
Sambamba na uzinduzi huo, Fatma alisema kutakuwa na ofa na promosheni nyingi, ikiwemo punguzo la asilimia 10% kwa mwezi huu mzima wa Novemba kwa mteja atakayenunua mzigo wa thamani kuanzia sh 200,000.
0 comments:
Post a Comment