Friday, 1 November 2019

BIDHAA ZILIZOISHA MUDA WA MATUMIZI,ZILIZOBADILISHWA LEBO ZAKAMATWA KWENYE MADUKA SHINYANGA MJINI

...
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga ikishirikiana na wakaguzi kutoka shirika la viwango TBS imefanikiwa kukamata shehena ya bidhaa zilizoisha muda wa zikiendelea kuuzwa katika maduka makubwa maarufu kama Supermarket mjini Shinyanga.

Bidhaa hizo zimekamatwa jana kutokana na msako katika maduka mbalimbali Mjini Shinyanga na kukamata shehena ya bidhaa mbalimbali ikiwemo chakula na vipodozi ambazo zimeisha muda wa kutumika vikiendelea kuuzwa madukani.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi huo,Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa Mhe. Jasinta Mboneko ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga amesema licha bidhaa nyingi madukani kuwa zimeisha muda wa kutumika pia wamebaini kuna udanganyifu mkubwa wa kubadilisha lebo za muda wa matumizi katika bidhaa mbalimbali ili ziendelee kuuzwa sokoni.

Naye Mkaguzi wa kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS Helen Andrew amesema operesheni hiyo sasa ni endelevu kwa mikoa yote.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa Mhe. Jasinta Mboneko akiangalia bidhaa ndani ya duka
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger