Sunday, 6 October 2019

Bunge Laiamuru Ikulu Ya Marekani Kutoa Nyaraka Zote Za Mawasiliano Ya Trump

...
Kamati za Bunge la Marekani zinazoendesha uchunguzi dhidi ya Rais Donald Trump zimeiamuru Ikulu ya Marekani (White House) kuwasilisha nyaraka zote za mawasiliano kati ya Rais Donald Trump na Ukraine

Amri hiyo imetolewa baada ya Ikulu ya Marekani kushindwa kuchapisha kwa hiari nyaraka hizo kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho uliokuwa umetolewa wa hadi Ijumaa

Mmoja wa viongozi wa Kamati za Bunge amesema ni wazi Rais Trump amechagua njia ya kuficha ukweli baada ya kushindwa kwa mwezi mzima kuweka wazi nyaraka za mawasiliano yake na Ukraine

Trump amesema huenda asitoe ushirikiano kwenye uchunguzi dhidi yake ambao unahusu madai kwamba alimshinikiza Rais wa Ukraine kumchunguza makamu wa Rais wa zamani, Joe Biden na mwanawe


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger