Monday, 28 October 2019

Waziri Lugola Aagiza Polisi Kuwakamata Wabadhirifu Wa Vyama Vya Ushirika

...
Na Felix Mwagara, MOHA, Bunda.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuwakamata viongozi wa vyama vya ushirika nchini ambao wamekuwa wakihujumu fedha za wakulima.

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo, katika Mkutano wa Viongozi wa Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, jana, kufuatia Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili kuwakamata viongozi wa vyama vya ushirika walioshindwa kurejesha fedha za Serikali zaidi ya bilioni moja na milioni mia nne atua ambayo imemfanya.

“Nawaagiza Polisi kuendesha operesheni ya kuwakamata wabadhirifu wa fedha na mali mbalimbali za umma, na agizo hili si la hapa Bunda tu, bali nchi nzima, makamanda wawasake na kuwatia mbaroni ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia hizo,” alisema Lugola.

Pia Waziri Lugola, alitoa onyo kali kwa viongozi wa vyama vya ushirika kote nchini kuwa Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara yake haitamuacha mtu salama atakayechezea fedha za Serikali.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili alisema wamewakamata viongozi wa vyama vya ushirika walioshindwa kurejesha fedha za Serikali na watawafikisha mahakamani.

“Fedha za vyama vya ushirika zimeliwa, tukaamua kuwakamata watuhumiwa wote na tayari tumefanya hizo, na tutawafungulia mashataka ili iwe fundisho kwa wananchi ambao wanatabia ya kuchukua fedha za umma,” alisema Lydia.

Waziri Lugola yupo Wilayani Bunda kwa ajili ya ziara ya kikazi, kuzungumza na wananchi, na pia kutatua kero mbalimbali zinazohusu Wizara yake Wilayani humo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger