Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Kepteni George Mkuchika amesema atawashughulikia wale wote anaohamisha watumishi vituo vya kazi kabla hawajathibitisha kwani ndio wanaochangia kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya Mikoa kuwa na upungufu wa watumishi.
Akizungumza Jijini hapa jana wakati akizindua Baraza Kuu la nne la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Kepteni Mkuchika amewataka utumishi wa Umma kutambua kuwa kila wakati wanapaswa kuwa tayari kufanya kazi mahali popote kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
Amesema katika ziara yake Mikoani amegundua Mikoa ya pembezoni ina uhaba mkubwa wa watumishi, akitolea mfano Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma ambayo ina watumishi chini ya asilimia 50.
Kuhusu suala la Rushwa, amesema taasisi zilizopo chini ya Ofisi Rais zinatakiwa kuwa kioo katika kukema vitendo vya rushwa, kwani Ofisi hiyo ndio inayoshughulikia wasiowaadilifu na si kujihusisha na vitendo hivyo.
Kwa pande wake Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Leah Ulaya amesema watumishi wa Umma wanajua kazi kubwa inayofanywa na Rais katika kuleta maendeleo kwa wananchi hivyo wataendelea kufanyakazi kwa weledi na uadilifu ili kuunga mkoni juhudi za Seriali.
Kuhusu malalamiko yaliyopo kwa watumishi wanaopandishwa madaraja lakini kiwango cha mshahara hakibadiliki,Wizara hiyo amewahakikishia kuwa suala hili litapatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo, huku ikimesema kuondolewa kwa watumishi 19,708 waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi kupitia zoezi la uhakiki kumeifanya Serikali kuokoa kiasi cha Sh 19.838 bilioni.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment