Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mjini Dodoma imemkamata mratibu wa mradi wa Belgian Fund for Food Security (BFFS) Wilaya ya Bahi, Emmanuel Mziwanda (62) kwa tuhuma za kuisababisha Serikali hasara ya Sh15 milioni.
Mkuu wa taasisi hiyo mjini humo, Sosthenes Kibwengo akizungumza leo Jumanne Oktoba Mosi, 2019 amesema mtuhumiwa huyo aliyekamatwa akiwa msibani alikuwa akitafutwa na taasisi hiyo tangu Julai, 2017 akikabiliwa na mashtaka ya kughushi nyaraka na kumdanganya mwajiri wake.
Amesema kitendo hicho kimeisababishia Serikali hasara ya Sh15 milioni na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika na mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kutoa kibali cha kumfikisha mahakamani, mtuhumiwa alitoweka kusikojulikana.
0 comments:
Post a Comment