Monday, 1 April 2019

Waziri Biteko Awasimamisha Kazi Maafisa Madini Ofisi Ya Madini Chunya

...
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko, ameagiza kusimamishwa kazi kwa wafanyakazi wote ofisi ya madini Wilayani Chunya na kuagiza  kuwafunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi na kwa tuhuma za kushirikiana na wachenjuaji wa madini.

Waziri Biteko ametoa kauli hiyo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya , wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika ukumbi wa halmashauri ya Chunya.

Amesema, baada ya serikali kupitia Wizara husika kuhakikisha inadhibiti mapato yake, utafiti umebaini kwamba Wilaya ya Chunya inashika namba moja kwa wizi na utoroshaji wa madini aina ya dhahabu ikifuatiwa na Kahama.

“Baada ya kufanya utafiti tumeabaini kunawizi mkubwa na usio na aibu ambapo unakuta mtu amepata kilo 1 na gramu 1620 lakini serikali inapata  gramu 208, lakini kuna mahali mtu anapata kilo nne anawasilisha taarifa za gramu 155,sasa wizi namna hii tukiendelea kunyamaza nchi haiwezi kuwa na afya.,”alisema.

Kutokana na hali hiyo Waziri Biteko  amewataka watendaji na viongozi husika kubadilika na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

“Ukiangalia sasa, wazalishaji wengi wanakimbilia Chunya na hii ni kwa sababu ya utaratibu wa eneo husika kushindwa kubaini wizi huu unaofanyika kupitia taarifa za kiwango cha uzalishaji ambacho ndicho kinachohalalisha mapato kwa serikali kupitia mrahaba wa Madini “Amesema Waziri Biteko

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, alimueleza Biteko kuwa Wilaya ya Chunya inahitaji msaada hasa wa kielimu na utaalamu wa madini na kuomba watendaji wasafi wapatikane kwenye sekta hiyo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa sasa wanataka kuzungumza na uongozi wa Mkoa  wa Songwe  ili kuunda nguvu ya pamoja itakayosaidia kuimalisha Ulinzi katika maeneo hayo ili kuepusha wizi wa Madini.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger