Wednesday, 24 April 2019

Serikali Yatoa Tamko Usajili wa Line za Simu Kwa Wasio na Vitambulisho Vya Taifa

...
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema  vyombo vya dola vitandelea kuimarisha amani na utulivu wa Tanzania ili kuhakikisha shughuli za maendeleo zinazoendelea hivi sasa.

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akitoa hoja kuhusiana na taarifa ya makadirio ya bajeti kwa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020, ambapo amesema atahakikisha amani inalindwa.

"Wizara itaendelea kulinda amani na usalama wa nchi hii kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wadau wengine, kuwepo kwa utulivu ambao watanzania wanauona utaendelea kuwezeshwa na hakika shughuli za maendeleo zitaendelea kuimarika." amesema Kangi

Aidha kuhusiana na zoezi la usajili walaini kupitia vitambulisho vya taifa, Waziri Lugola amesema watanzania milioni 16 ambao wana namba za vitambulisho vya NIDA wana sifa za kusajili kadi za simu ya mkononi   na wasio na vitambulisho hivyo watawekewa utaratibu maalum.

“Mtanzania huyu tutampa utaratibu kwa sababu si kosa lake kutosajiliwa simu kwa sababu Serikali tupo kwa ajili ya kuwalinda Watanzania.

“Watanzania hawapaswi kuwa na maisha ya wasiwasi, lazima waendelee kutumia simu kuanzia anainunua mpaka pale atakapoacha kuitumia. Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa) tulikuwa na lengo la kutambua na kutoa vitambulisho milioni 24.5, hayo ndiyo malengo.

“Lakini mpaka sasa Nida tumekwishafanya utambuzi, usajili wa Watanzania wenye sifa milioni 16, tulipoona kwamba wenzetu wa TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania)  wanataka kubadilisha masuala ya kusajili simu ili waweze kutumia alama za vidole na kwamba mwenye kitambulisho cha taifa ndio atakayesajiliwa,sisi kupitia Nida tuliweka utaratibu.

 “Watanzania  ambao wamekwishapata vitambulisho watatumia  vitambulisho vyao. Watanzania milioni 16 tayari wameshapatiwa namba inaitwa NIN yaani National Identification Number, kwa hiyo namba hiyo ambayo anasubiri apewe kitambulisho chake ndiyo atakayoiwasilisha NIDA,” amesema.

Lugola amesema namba hiyo itawasilishwa TCRA na mhusika ataitumia kusajiliwa.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger