Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Kikao cha Kamati Kuu kimemteua Ngugu, John Danielson Pallangyo kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Arumeru.
Tume ya Uchaguzi ilitangaza uchaguzi wa marudio kuwa ni Mei 19 na Jimbo la Arumeru Mashariki lilikuwa wazi baada ya aliekuwa Mbunge wake Joshua Nassari kuvuliwa ubunge na Spika kutokana na kutohudhuria vikao vitatu.
Chama cha Mapinduzi kimefanya Kikao cha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa NEC jana mchana jijini Dodoma wakiogozwa na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.
0 comments:
Post a Comment