Monday, 15 April 2019

Msimu Wa Tatu Wa “Smirnoff Ice Black Dj Search” Wamalizika, Washindi Wajizolea Zawadi

...
Dar es Salaam. Aprili 14, 2019. Hatimaye msimu wa tatu wa wa shindano la ‘Smirnoff Ice Black Dj Search’ kwa mwaka 2019 umemalizika huku DJ KG akiibuka mshindi kwa kuwapiku maDj sita walioshiriki kwenye fainali hizo.
 
DJ KG kutoka Mkoa Dar es Salaam alitangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa shindano hilo ambapo jumla ya maDJ sita walishiriki na kudhaminiwa na kinywaji cha Smirnoff Ice Black kinachozalishwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).
 
Akizungumza wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbu wa Life Park Mwenge, Meneja wa bidhaa wa SBL Ester Raphael alisema lengo ni kuibua vipaji vipya kweye tasnia ya muziki kupitia fani ya uburudishaji ‘DJ’ sanjari na kutoa hamasa kwa wateja wa bidhaa zao.
 
“Tunaamini kwa kupitia shindano hili, SBL itatoa msisimko kwa wateja wake na muziki mzuri na nafasi ya kipekee kuonyesha uwezo wa MaDj wanaochipukia,” alisema
 
Shindano hilo limefanyika katika mikoa mitano ikiwamo Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Mwanza na Arusha ambapo waliweza kuwapata maDj sita waliotinga hatua ya fainali.
 
Alitaja zawadi zinazotolewa kwa washindi ikiwamo vifaa vya Dj “Dj Kit,Laptop pamoja na Conrollers kwa washindi watatu.
 
“Ushindani wa msimu huu ni mkubwa sana na tumeona Madj wakipamana kwa hali na mali na hamasa imekuwa kubwa sana kwao na kwa wateja wa kinywaji chetu cha Smirnoff Ice Black,” alisema
 
Katika fainali hizo, DJ KG kutoka Mkoa wa Dar es Salaam aliibuka mshindi wa kwanza na kuibuka na DJ kits pamoja na Laptop (Mac). Mmoja wa Majaji, Immanuel John ‘DJ Summer Tz’ alisema walizingatia zaidi ujuzi wa DJ pamoja na muitiko kutoka kwa watu wanaowasikiliza.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger