Mashindano ya Riadha yenye Jina ‘Monduli Maasai Marathon’ yanatarajiwa kufanyika June 29, mwaka huu mjini Monduli mkoani Arusha.
Mratibu wa Mashindano hayo Cletus Pius Wilbert "Big Daddy" amesema mashindano hayo yataanzia eneo la uwanja wa Polisi kuzunguka raundi tatu kisha kuishia Uwanjani hapo.
Big Daddy amesema kutakuwa na mbio za kilomita 2.5 zilizopewa jina Nyangulo Run, Km 5 Laigwanani Run huku Km 21 zikiwa ni Morani Run na washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali akiwemo Ng’ombe mkubwa na mgeni rasmi ambaye atatangazwa baadaye.
Amesema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri ambapo kwa sasa kamati inaendelea kutafuta wadhamini mbalimbali ili kuweza kufanikisha zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa.
Big Daddy amesema lengo kubwa la mashindano hayo ni kutangaza wilaya ya Monduli ambayo ina fursa mbalimbali za utalii ambazo zinaweza kusaidia kuingeza mapato katika Hlamashauri lakini pia kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao na kufufua riadha wilayani Monduli.
"Mashindano haya yanaandaliwa na LIVE HIGH COMPANY kwa kushirikiana na CAS MICROFINANCE LTD.,Tmeaandaa zoezi hili ili kuitambulisha wilaya ya Monduli na fursa zilizopo",amesema.
Amesema Mbio hizo zitakazofanyika Monduli Mjini katika uwanja wa Polisi zitashirikisha washiriki mia tano [500] kutoka rika mbalimbali wakiwemo vijana, watoto, wazee yakisindikizwa na kauli mbiu ‘MONDULI PAZURI, TAMBUA FURSA ZILIZOPO’.
0 comments:
Post a Comment