Kampeni ya unywaji wa kistarabu inayoendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) imezinduliwa rasmi Mkoani Arusha huku madereva wa vyombo vya moto wakihimizwa kuzingatia sheria za barabarani ikiwamo kutotumia vilevi wakati wa kazi.
Kampeni hiyo maarufu kama ‘Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto’ imeenda sambamba na ugawaji wa makoti ya usalama (Reflectors) kwa madereva bodaboda mkoani humo ikiwa ni mkakati wa kuhimiza matumizi ya vifaa hivyo kwa usalama wa watumiaji wa barabara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika leo katika Makao Makuu ya Traffic jijini hapa, Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha amesema kampeni hiyo imelenga kutoa elimu kwa wateja wake nchini ili kupunguza matukio yanayoepukika kama ajali zitokanazo na unywaji wa pombe kupindukia.
“Pombe isipotumika kiistarabu inaweza kuleta madhara katika jamii na mojawapo ya madhara ni pale mtu anapokunywa pombe na akaendesha chombo cha moto ikasababisha ajali jambo ambalo ni hatari kwa madereva na pia ni hasara kwa Taifa,” alisema
Kampeni hiyo inashirikisha wadau mbalimbali ikiwamo Jeshi la Polisi-Kikosi cha usalama barabarani, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), madereva bodaboda pamoja na jamii kwa ujumla ikilenga katika kupunguza ajali zitokanazo na ulevi wa kupindukia nchini.
Kwa upande wake,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO) Joseph Bukombe alisema kampeni hiyo itasaidia katika kupunguza ajali zinazosababishwa na ulevi huku akiwataka madereva kuzingatia kuacha kutumia vilevi ili kujihakikishia usalama wawapo barabarani.
“Unywaji wa pombe kiistarabu ni suala la muhimu sana kwa madereva kwasababu madereva wakiwa kwenye hali ya ulevi ni moja ya chanzo cha ajali za barabarani hivyo tunaipa kipaumbele kampeni hii hapa mkoani Arusha na tutaendelea kutilia mkazo suala hili,” alisema
Aliipongeza SBL kwa kuona umuhimu wa kuwalinda watumiaji wa barabara kwa kutoa elimu hiyo kwa madereva na umma kwa ujumla.
“Pamoja na kuwa wao (Serengeti) ni watengenezaji wa pombe lakini wameona wajibu wao wa kumlinda na kuleta usalama wa madereva na watumiaji wengine wa barabara,” alisema
Kwa mujibu wa ripoti za Jeshi la Polisi-Kikosi cha Usalama barabarani kwa mwaka 2018, jumla ya ajali 876 za bodaboda ziliripotiwa kutokea na kusababisha vifo 366 na majeruhi 694. Ripoti zinaonyesha kupungua kwa ajali hizo ambapo kwa mwaka 2017 zilikuwa 1,459 zilizosababisha vifo 728.
MWISHO
Kuhusu SBL:
Ikiwa imeanzishwa kama Associated Breweries mwaka 1988, Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) ni moja ya kampuni kubwa za bia nchini Tanzania, ambapo aina zake za bia zinachangia zaidi ya asilimia 20 ya bidhaa hizo katika soko.
SBL inaendesha viwanda vitatu vilivyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.
Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara yake imekua na kuimarika zaidi na asilimia 51 ya hisa mwaka 2010 zilizochukuliwa na Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) zimeshuhudia ongezeko la uwekezaji katika kukua zaidi na hivyo kusababisha kuongezeka kwa fursa zaidi za ajira kwa watu wa Tanzania.
Aina za bia zinazozalishwa na SBL ambazo zimepata tuzo kadhaa za kimataifa ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick.
SBL pia ni wazalishaji vinywaji vikali vinavyofahamika duniani kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum na Baileys Irish Cream.
Kwa habari zaidi wasiliana na:
John Wanyancha,
Mkurugenzi wa Mawasiliano, SBL
Simu: 0692148857
Barua pepe: john.wanyancha@diageo.com & Imani Lwinga:Meneja wa Mawasiliano, SBL Tel: 0785428282 Email: Imani.lwinga@diageo.com
0 comments:
Post a Comment