Wednesday, 17 April 2019

Bunge la Iran latangaza vikosi vya jeshi la Marekani katika Mashariki ya Kati kuwa la kigaidi

...
Wabunge wa Iran kwa kauli moja wamevitangaza vikosi vya jeshi la Marekani katika mashariki ya kati kuwa ni vya kigaidi siku moja baada ya uamuzi wa Marekani kuliweka jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya Iran kuwa la kigaidi kuanza kufanyakazi rasmi. 

Waziri wa Ulinzi Jenerali Amir Hatami amewasilisha mswada huo unaoidhinisha serikali kuchukua hatua kali katika kujibu hatua za kigaidi za jeshi la Marekani. 

Mswada huo unataka maafisa kutumia hatua za kisheria, kisiasa na kidiplomasia kuzuwia hatua za Marekani, lakini hakutoa maelezo zaidi. 

Hatami amewaambia wabunge kwamba hatua ya Marekani inayo lenga kuzuwia ushawishi wa Iran, inaonesha kwamba vikwazo vya muda mrefu vya Marekani dhidi ya Iran havijaleta athari. 

Katika mjadala huo baadhi ya wabunge wenye msimamo mkali walitaka kuliorodhesha jeshi zima la Marekani na majeshi ya usalama kuwa ni ya kigaidi.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger