Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limeua watu watatu kwa tuhuma za ujambazi. Inadaiwa watu hao walikuwa na silaha ya moto ambayo haijafahamika ni ya aina gani katika maeneo ya Nyakabungo Kata ya Isamilo wilayani Nyamagana. Kaimu Kamanda wa jeshi hilo mkoani Mwanza Advera Bulimba, alithibitisha kuuawa kwa watuhumiwa hao, huku akifafanua kuwa wengine watatu wanasadikika kutokomea kusikojulika. Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nane usiku, baada ya askari kupokea taarifa toka kwa raia wema kuwa katika maeneo hayo kunasikika milio ya risasi ambayo ilikuwa inaashiria kuwapo kwa uvunjifu…
0 comments:
Post a Comment