
Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha katika ajali iliyohusisha magari aina ya Canter lenye namba za usajili T223ATK na Hiace yenye namba za usajili T869 GHT kugongana katika Mlima Nyangoye eneo la Hamugembe Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Ajali hiyo imetokea usiku huu Februari 8,2019
Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuna taarifa ya vifo vya abiria,idadi haijulikani na bado mamlaka husika hazijazungumzia tukio hilo.
Malunde1 blog inaelezwa kuwa Hiace /daladala yenye Jina la Kitunze Kidumu inayofanya safari zake Bukoba - Mtukula ilikuwa inaelekea kupaki.
Taarifa Kamili tutawaletea hapa Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment