Friday, 15 February 2019

Airbus kusitisha uzalishaji wa ndege zake aina ya A380

...
Shirika la Airbus limetangaza kwamba ifikapo mwaka 2021 litasitisha uzalishaji wa ndege zake aina ya A380 superjumbo kutokana na kukosekana kwa soko.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shirika hilo ifikapo mwaka 2021 oda zilizokuwepo za ndege aina ya A380 zitakabidhiwa kwa wanunuzi na uzalishaji wa ndege hizo utasimamishwa.

Katika taarifa hiyo mkurugenzi mkuu wa Airbus Tom Enders alisema, wanatoa tangazo hilo huku wao na wanahisa wengine wa A380 wakiwa na uchungu.

Mteja mkuu wa ndege hizo aina A380 shirika la ndege la Emirates limepunguza kiasi cha manunuzi ya ndege hizo kutoka ndege 162 hadi 123 imefahamishwa katika taarifa hiyo.

Emirates imeingia mkataba mpya wa kununua ndege 70 aina ya A330-900s na a350-900s mbadala wa A380. Mkataba huo mpya una thamani ya dola bilioni 21.4.

Ndege hizo za Airbus A380 zenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 800 ziliazalishwa kutoa ushindani kwa ndege aina ya Boeing 747 za shirika la uzalishaji ndege la Marekani.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger