Wednesday 25 January 2017

NACTE YAANZA KUPOKEA MAOMBI YA WANAFUNZI WANAOTAKA KUJIUNGA NA VYUO VYA AFYA,UALIMU,MIFUGO,KILIMO ETC NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 -MARCH /APRIL INTAKE

...
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)

TAARIFA KWA UMMA

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yaani “Online Central Admission System (CAS)”, umefunguliwa rasmi tarehe 23 Januari, 2017, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada na Stashahada kwa Kipindi cha Machi/April, 2017 kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Namna ya Kufanya Maombi
Maombi yote yafanyike kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) au kupitia chuoni ambapo mwombaji anapendelea kwenda kusoma, ambapo chuo kitamdahili mwanafunzi husika kwenye mfumo wa udahili kupitia “Institutional Panel”.

Tanbihi: Waombaji wa kozi za Afya waliohitimu Astashahada (NTA Level 5), pia wataomba kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.
Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo:
  1. Biashara, Utalii na Mipango, mfano; Uhasibu, Meneja Rasilimali Watu, Wanyama Pori, Mipango.
  2. Sayansi na Teknolojia Shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya Mawasiliano, Usanifu Majengo, Mifugo.
  3. Afya na Sayansi Shirikishi, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi.
Sifa za muombaji
  1. Awe amehitimu kidato cha nne mwaka 2015 au kabla ya hapo.
  2. Awe na Astashahada ya mwaka 2016 au kabla ya hapo kwa wanaojiendeleza.
  3. Sifa kwa kozi mahsusi ziko kwenye mwongozo wa kozi (Guidebook) ulioko kwenye mfumo (CAS).
Ada ya maombi ni kama ifuatavyo:
  1. Kwa eneo la Afya na Sayansi Shirikishi ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
  2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=.
  3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Biashara, ada ni Tshs 30,000/=, ambapo muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 06/03/2017.

Muhimu: Hakutakuwa na muda wa nyongeza wa kufanya maombi. Hivyo waombaji wanashauriwa kuwa makini wakati wa kufanya maombi yao.

Angalizo: Kwa eneo la Mafunzo ya Ualimu na kozi ya Muhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (Community Health Workers) hayatakuwepo kwenye udahili wa awamu hii.







Imetolewa na: 
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
23 Januari, 2017
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger