Tuesday 24 January 2017

WALIMU WATATU WAKAMATWA KWA KUPIGA DILI LA KUPOKEA MISHAHARA PRIVATE NA SERKALINI

...
Walimu watatu mkoani Mwanza wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la  kukimbia vituo vyao vya kazi na kufanya kazi shule binafsi huku wakiendelea kupokea mishahara ya serikali

Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Mwanza imewataja walimu hao waliokamatwa jana asubuhi katika mtaa wa Buhongwa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,kuwa ni pamoja na Richard Mgendi (30), Rwiza Ntare (27) na Gilbert Makwaya (33).

Walimu hao kila mmoja ana story yake kama ifuatavyo:-

Mwalimu Richard Mgendi alikuwa akifundisha shule ya sekondari ya Misasi wilayani Misungwi, mwaka 2012 alimuaga mkurugenzi wa wilaya hiyo kuwa anakwenda kusoma Masters ya lugha (Linguistic) katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino, kwa kipindi chote hicho inadaiwa mwalimu huyo alikwenda kusoma na alipomaliza hakurudi katika shule yake ya awali bali alikuwa akifundisha shule binafsi ya sekondari iitwayo Musabe iliyopo Buhongwa huku akiendelea kulipwa mshahara kutoka serikalini.

Mwalimu Rwiza Ntare alikuwa akifundisha shule ya sekondari iitwayo Kigongo sekondari iliyopo wilaya ya Chato mkoani Geita ambapo mwaka 2015, alimuaga mkurugenzi wake kuwa anakwenda hospitali ya rufaa ya Bugando kupatiwa matibabu ya macho na vidonda vya tumbo lakini hakurudi tena bali inadaiwa alikuwa akifundisha shule binafsi ya sekondari iitwayo Musabe iliyopo mtaa wa Buhongwa huku akiendelea kulipwa mshahara na serikali.

Mwalimu Gilbert Makwaya alikuwa akifundisha Runima sekondari iliyopo maeneo ya Buhongwa na alimuaga mkurugenzi wa wilaya ya Nyamagana tarehe 27/09/2015 kuwa anakwenda kusoma Masters ya Hesabu katika chuo kikuu cha Mwenge kilichpo mjini Moshi lakini hakwenda bali alikuwa akifundisha shule binafsi ya Musabe iliyopo mtaa wa Buhongwa huku akiendelea kupokea mshahara kutoka serikalini.

Walimu wote watatu wapo katika mahojiano na jeshi la polisi na pindi uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Jeshi la polisi linaendelea kuwatafuta baadhi ya walimu ambao wametoroka lakini inadaiwa wapo katika shule hiyo binafsi ya Musabe huku wakiendelea kulipwa mshahara na serikali pamoja na mkurugenzi wa shule hiyo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger