Friday 27 January 2017

Mkuu wa Wilaya ajiuzulu, amwandikia barua Rais Dkt Magufuli

...
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Uyui Bw.Gabriel Mnyele akizungumza na Mwandishi wa habari wa Azam tv Juma Kapipi wakati akiwa ofisi za CCM Wilaya ya Uyui ikielezwa kuwa alikuwa ameitwa na Uongozi wa chama hicho kufuatia kuwepo kwa taarifa kwamba ameamua kuachia ngazi nafasi ya Ukuu wa wilaya hiyo ya Uyui jambo ambalo alilithibitisha kwa Katibu wa CCM wilaya ya Uyui kwamba ni kweli amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli. 

 *****
Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gabriel Simon Mnyele amejiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi Januari 26, 2017 na kuwaaga madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano alioufanya wilayani humo.

Akieleza sababu ya kufanya uamuzi huo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa alimwandikia Rais Dkt Magufuli barua ya kujiuzulu nafasi hiyo akielezea kusongwa na majukumu binafsi.

Mkuu wa Wilaya, Gabriel Simon Mnyele alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 26 Juni, 2016.
Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka Waandishi waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu."Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe,kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?Aliwahoji waandishi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger