Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana July
30 2016 ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoa wa
Singida.
Mkoani
Tabora, Rais Magufuli alizungumza na wananchi waliosimamisha msafara
wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na alifanya mikutano ya hadhara
Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake
itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya
Mwaka 2015.
Katika
mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea
malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na
soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha
mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu
ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.
Kuhusu
kero ya maji, Dkt. Magufuli alisema Tanzania imepata mkopo wa dola za
kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika
kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya
Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge
Rais
Magufuli na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Masesa
Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea Nzega
Mkoani Tabora.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na wabunge wa Singida
Rais Magufuli katika Kijiji cha Nanga Wilayani Igunga mkoani Tabora.
0 comments:
Post a Comment