July 31 2016 mwili wa marehemu Mwanahabari Joseph Senga umeagwa
Dar es salaam leo kuelekea Mwanza kwa ajili ya maziko, baadhi ya
viongozi wa serikali na siasa wameshiriki wakiwemo Waziri wa habari,
utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye, Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa na wengine.
Marehemu Joseph Senga ndiye mpiga picha aliyenasa tukio la mauaji ya Mwandishi wa habari wa kituo cha talevisheni CHANEL 10 Daud Mwangosi kilichotokea September 2 2012 katika kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambaye alifariki July 28 2016 akiwa India kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Ninazo picha kadhaa kutokea Sinza Dar es salaam ambapo ndipo kazi yote ilifanyika

Hii hapa chini ni moja ya picha yake enzi za uhai

Marehemu Joseph Senga ndiye mpiga picha aliyenasa tukio la mauaji ya Mwandishi wa habari wa kituo cha talevisheni CHANEL 10 Daud Mwangosi kilichotokea September 2 2012 katika kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambaye alifariki July 28 2016 akiwa India kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Ninazo picha kadhaa kutokea Sinza Dar es salaam ambapo ndipo kazi yote ilifanyika

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye

Kutoka kushoto Edward lowassa, Nape Nnauye na Freeman Mbowe

Mke wa marehemu Joseph Senga (aliyevaa ushungi)

Wapigapicha na wanachama wa Press Photographer wakishiriki kubeba jeneza la marehemu

0 comments:
Post a Comment