Pia Mheshimiwa Simbachawene aliziagiza mamlaka zinazohusika na kuwapokea
wanafunzi wapya wa kidato cha tano kuhakikisha kuwa miundombinu yote
muhimu inakamilika ikiwemo mabweni, madarasa vyoo na Maabara, samani
(vitanda, Meza na Viti huduma za Maji na Umeme zinatekelezwa na
kukamilika kwa wakati.
Katika mwaka 2016 jumla ya shule mpya za kidato cha tano 50 zimeanzishwa
kutokana na maombi ya mikoa kwenye maeneo yao ili kuendana na lengo la
Serikali la kuongeza Shule za Kidato cha Tano na Sita.
Hivyo, Waziri Simbachawene amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa shule zote zina walimu na
vitabu vya kujifunzia na kufundishia na pia kuhakikisha chakula kwa
wanafunzi wa bweni kinaandalaiwa kabla wanafunzi wapya wa kidato cha
tano hawajaripoti.
0 comments:
Post a Comment