MTUHUMIWA wa ujambazi Msafiri Suleiman maarufu kama Juma Msukuma ameuawa wakati akijaribu kuwatoroka Polisi.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa tukio hilo
lilitokea Julai 28 mwaka huu majira ya saa 10.30 jioni katika eneo la
Igoma kata ya Igoma jijini Mwanza.
Kamanda
Msangi alisema mtuhumiwa siku hiyo alikuwa amekamatwa na Polisi
akituhumiwa kufanya matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha
akishirikiana na wenzake watatu.
Aliwataja
watu hao aliokuwa akishirikiana nao ambao kwa sasa wamekamatwa na
polisi kuwa ni Jackson Magesa ( Nyakibimbi), Samwel Mwita na Boniphace
Nyamhanga.
Kamanda
alisema baada ya mahojiano na polisi mtuhumiwa alikiri kuhusika na
uhalifu na akakubali kwenda kuwaonesha askari sehemu aliyoficha silaha
maeneo ya Buhongwa mlimani.
Alisema
walipofika eneo husika aliwaonesha mkasi mkubwa wa kukatia vyuma na
kipande cha nondo, huku akiwathibitishia kuwa silaha alikuwa ameichimbia
ardhini katika eneo hilo.
“Wakati
askari wakiwa kwenye harakati za kufukua ili waichukue silaha hiyo,
mtuhumiwa alitumia mwanya huo kuanza kukimbia huku akiwa na pingu
mkononi, askari walifyatua hewani risasi tatu, lakini mtuhumiwa hakutii
amri hiyo ndipo alipopigwa risasi mguuni na kufanikiwa kukamatwa”, alifafanua.
Alisema alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali.
“
Watuhumiwa aliokuwa akishirikiana nao tumewakamata na tumewakuta wakiwa
na bunduki aina ya Rifle Mark 4 ikiwa na risasi nne, ikiwa na kitako
cha bunduki waliyopora, nyundo moja na vipande vitatu vya nondo”, alisema.
“
Watuhumiwa hao tunawashikilia kwa matukio ya unyang’anyi Nyashishi,
Buhongwa, Bulale, Nyambichi na Mwananchi ambapo walipora silaha toka kwa
mlinzi wa Kampuni ya Paroma Patrol Security Service”, aliongeza
0 comments:
Post a Comment