Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani,
Papa Francis amepata ajali ya kuanguka ghafla alipokuwa akitembea
kuelekea kwenye jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuendesha ibada,
Czestochowa nchini Poland.
Papa Francis mwenye umri wa miaka 79
alisaidiwa kwa haraka na wasaidizi wake na kufanikiwa kuamka na
kuendelea na safari hadi kwenye kiti kilichoandaliwa.
Papa Francis alikosa kukanyaga vyema
kidato kimoja na akaanguka katika madhabahu matakatifu zaidi nchini
humo, madhabahu ya Jasna Gora.
Papa, mwenye umri wa miaka 79, mzaliwa
wa Argentina, alionekana akitembea akiwa anatafakari sana, na hakugundua
kulikuwa na kidato kimoja kabla ya kufikia altare, shirika la habari la
AP limeripoti.
Mapadre waliokuwa karibu naye walikimbia na kumsaidia kuinuka.
Misa iliendelea kama ilivyopangwa na
papa alihubiri kwa muda mrefu mbele ya maelfu ya waumini waliokusanyika
Jasna Gora katika jiji la Czestochowa, kusini mwa nchi hiyo.
Ibada hiyo ilikuwa ikirushwa moja kwa moja kupitia vituo mbalimbali vya runinga na kuangaliwa na mamilioni ya watu.
Shirika la habari la AFP linasema aliinuka upesi, na hakuonekana kuumia hata kidogo.
Alipoulizwa iwapo Francis aliumia baada ya kuanguka, msemaji wa Vatican Greg Burke ameambia wanahabari “papa yuko salama”.
Papa amewahi kuteleza na hata kuanguka
mara kadha awali, na kila mara huwa anainuka peke yake au kusaidiwa na
mmoja wa wasaidizi wake, shirika la AP linasema.
Kwa mujibu wa Daily Mail, Papa Francis
anasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kama Sciatica, ugonjwa ambao wakati
mwingine hushusha maumivu ya ghafla kwenye miguu kutoka mgongoni.
Angalia Video hapa
0 comments:
Post a Comment