Katika kuonyesha jinsi ambavyo wananchi wengi wanakubaliana na mtazamo na mwelekeo wake katika hatma ya Taifa, Mwenyekiti wa CHADEMA amewaomba sana walinzi wa Rais ili asalimie Rais kwa sababu anachokifanya Rais kinamgusa katika hali chanya kimaisha na kitaifa.
Rais baada ya kuona tukio hilo aliwaomba walinzi wake kama kuna uwezekano wamruhusu.
Rais Magufuli amezungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na amefanya mikutano ya hadhara Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.
Kuhusu kero ya maji, Dkt. Magufuli amesema Tanzania imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Ndugu Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea Nzega Mkoani Tabora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Ziba Wilayani Igunga mkoani Tabora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wakazi wa Igunga mkoani Tabora katika ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo wa Tabora
Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo.
0 comments:
Post a Comment