Friday, 22 July 2016

MPYA:USHAURI KOZI ZA KUCHAGUA KWA FORM SIX COMBINATION ZA PCB,PCM,CBG,HKL,HGK,HGL,EGM,HGE NA PGM

...
 Image result for TCU.GO.TZ
Habari yenu?
Kutokana na wadau weng kuuliza kuhusu ushauri wa kozi gani za kuchagua kutokana na matokeo aliyopata,nimeamua kuweka hapa ushauri ambao naamini kwa asalimia zaidi 90% nitagusa kila mtanzania,mwenye haja ya kujua haya mambo.

KAMA ULISOMA PCB/CBG

 PCB ni moja ya combination ambayo inajumuisha masomo ya PHYSICS,CHEMISTRY NA BIOLOGY.Wengi wa wanafunzi wanaoenda kusoma masomo haya a level,ndoto zao ni kuwa madaktari,wafamasia,lab technologist na nursing.

Ukweli ni kwamba baada ya matokeo ya kidato cha sita malengo ya wengi huwa yanapotea kutokana na kupata maksi ambazo haziridhishi kwenda chuo kikuu kusomea masomo hayo ya afya.

Nina recommend:kama umepata PCB DIV III pts 13 kwenda-14,15 etc.Ninakushauri usisumbuke kuomba MEDICINE/PHARMACY hii inawahusu wote wenye D D,C E, kupata kozi hizo ni ngumu sana kwa vyuo vya MUHIMBILI,BUGANDO,KCMC,UDSM sio kwamba hauna sifa,sifa unazo ila tatizo ni competition.

Note:medicine CBG hawapokei,so nakuomba usijisumbue kuomba.

Ninakushauri uombe kozi za kilimo -zilizopo SUA kama agronomy,agri general,hortculture,aqualculture,animal science,food science and technology,human nutrition etc.zipo pale sua.

Nursing:Vile vile kama hauna matokeo mazuri ya form six ninakuomba usiombe kozi hii,hii ni kutokana na competition.

Ninakushauri kama kwenu wanuwezo wa kukulipia ada ya kuongezea omba chuo cha KAMPALA UNIVERSITY lakini ada yake ni kubwa sana.

Ushauri wangu huu nakuomba uuzingatie kwa umakini sana hii ni kutokana na KUFUTWA KWA KOZI ZA MEDICINE UDOM,IMTU,ST.JOSPEH,ST.FRANCIS maana yake competition itakuwa ni kubwa sana.

hivyo kukufanya wewe ukose chuo.

Pia unaweza kutazama tcu guide book course mbalimbali mpya zitolewazo hapa tanzania,lakini kwa swala la MEDICINE/PHARMACY/NURSING ni ngumu kupata kutokana na matokeo hayo.

 
MADHARA YA KUKOSA CHUO AWAMU YA KWANZA

Endapo hutazingatia ushauri wangu na ukachagua kozi hizo za afya na wakati ufaulu wako ni mdogo sana,utakosa chuo baada ya hapo,itakulazimu uchague kozi mpya kutoka kwenye vyuo vingine ambavyo vitakuwa vinanafasi.
Hapo ndipo ndoto za wengi hupotea kutokana kulazimika kusoma kitu mabacho hikupendi.FANYA MAAMUZI SAHIHI SASA,KABLA HUJAKOSA FISRT ROUND.

Mwaka jana walikosa zaidi ya wanafunzi 13,000 fisrt round.

 NITAENDLEA..........
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger