Sunday 24 July 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 1 & 2

...



Mtunzi:Eddazaria G.Msulwa
Ni siku ya jumamosi kama kawaida wanafunzi wote wa shule tunayosoma tunakwenda viwanjani kucheza michezo mbali mbali kama mpira wa miguu na michezo mingine ambayo wanacheza wasichana waliopo katika shule yetu ambayo niya bweni yenye mchanganyiko wa wasichana na wavulana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na nishule ya mtu binafsi(PRIVET SCHOOL) iliyopo katoka mkoni Arusha.
Kama kawaida yangu ya kuwa shabiki wa timu ya darasa langu la kidato cha tano ninachosoma ninaendelea kutazama mechi tunayocheza na kidato cha tatu hadi wakati huu tumeshafungwa goli mbili kwa moja huku dakika zikiwa zinakimbia kuelekea ukingoni huku mashabiki wa kike wa kidato cha tano wakiendelea kuwapa moyo wachezaji wetu waliopo uwanjani

“Oya Eddy mcheki yule manzi pale”
“Yupi?”
“Yule aliyevaa sweta jeupe”
“Ana nini?”
“Cheki alivyo bomba majamaa kibao wamemtokea wamepigwa chini”
“Yupo kombi gani?”
“HKL”
“Ndio maana angekuwa huku tulipo sisi wala asingekuwa mzuri”

“Hembu acha pumba zako Eddy”
“Kweli John unadhani angekuwa science unadhani angekuwa hivi wewe si unawaona wakina Matha walivyo kauzu class hadi kuwatongoza mtu unashindwa”

Tukajikuta tukikatisha mazungumzo baada ya mchezaji wetu mmoja kufunga bao la kukomboa jambo lililoturudishia furaha hata ya kuwepo uwanjani.

Kabla hata ya dakika mbili mbele mchezaji wetu yule yule akafunga bao jingine kupitia mpira wa kona uliopigwa na akaudumbukiza nyavuni kwa kichwa na kuamsha shangwe za wanafunzi wote wa kidato cha tano na kuwafanya mashabiki baadhi kuingia uwanjani huku wakishangilia kwa furaha kwani tayari dakika zilisha kwisha.

Mimi na rafiki yangu John tukabaki nje ya uwanja huku sura zetu zikiwa na furaha kupita maelezo

“Wee dada jamaa anakuita hapa”.John alimuita yule msichana tuliyekuwa tunamjadili dakika kadhaa zilizopita.

Akatuangalia kwa dharau yeye na rafiki zake kisha wakaongea maneno ya kunong’onezana na kuanza kucheka kicheko kilichotufanya tuwe kimya kama tumemwagiwa maji ya baridi.

Safari ya kurudi shuleni ikaanza kwani kiwanja chetu cha mpira kipo eneo la nje ya eneo la shule.Tukiwa tumeongozana na kundi la wasichana wa kidato chetu wakiimba nyimbo za ushindi mimi na John tukawa na kazi ya kumfwatilia yule msichana ambaye kusema la ukweli amejaliwa uzuri unaweza kusema alipewa siku yake ya pekee katika uumbwaji wake

Tukafika hadi kwenye duka la shule ambapo yule msichana alikwenda na rafiki yake ambaye kidogo naye anavutia japo si sana.Kutokana hatukuwa na lengo la kufika katika duka hilo kwa aibu tukajikuta tukinunua mifuko miwili ya pipi za Big boom

“Claudia ile hela siioni” Yule msichana alizungumza huku akiwa anajipapasa papasa kwenye mifuko ya sketi yake huku akionekana kuwa na wasiwasi wa hali ya juu kwani tayari walishakunywa soda pamoja na kula keki za watu

“Hebu tazama vizuri”
“Kweli si unaona mifuko yote haina hela jamani sijui imeangukia wapi”

Nikawatazama kwa huruma kisha nikatoa waleet yangu mfukoni iliyotuna kwa wingi wa pesa nikamuuliza muuza duka ni kiasi gani cha pesa anachowadai akaniambia nikawalipia na chenchi iliyobaki nikamwambia muuza duka awapatie.

Tukaanza kuondoka kabla hatujafika mbali Claudia akatuita na tukasimama wakaja katika lile eneo tulilosimama huku rafiki yake ambaye ndio aliyetufanya twende pale dukani kwa kumfatilia akaawa analia

“Samahani kaka zangu tunawashukuru”

“Haina shida vitu vya kawaida,Eddy twende zetu”

“Ngojeni kwanza”

Claudia alizungumza huku akimshika John beda aliyeanza kugeuka na kutaka kuanza kuondoka katika eneo tulilo kuwepo

“Mbona huyo mwenzako analia”

 “Amepoteza pokety money yake ndio kwanza ametoka kuipokea leo mchana kwenye basi”

“Mmmm poleni”

John alizungumza kwa maringo na kuanza kuondoka ikanilazimu mimi kubaki kwani roho ya huruma ilianza kunitawala huku wakati wote nikimtazama yule msichna ambaye bado sikulitambua jina lake

“Amepoteza sh ngapi?”

“Eti Salome umepoteza shii ngapi?”

“Elfu themanini na tano”

Nikakaa kimya kama dakika mbili nikifikiria nini nifanye,nikajikuta nikiitoa wallet yangu mfukoni na kuesabu noti tisa za elfu kumi kumi kisha na kuzitoa na kumpa Salome taratibu akazipokea huku akiwa haamini tukio linalo tendeka kwa wakati huo.

“Zitakusaidia saidia siku mbili tatu”

“Asante sana kaka yangu”

“Powa ukiwa na shida utakuja darasa la PCB ndio ninaposoma”

Nikawapa na mfuko wa pipi nilio nunua kisha nikaondoka huku moyoni mwangu nikijifariji kuwa tayari nimesha fanikiwa katika hatua ya kwanza ya kumpata mtoto mzuri.

Tukafika bwenini tukaoga kujiandaa na sikukuu ya wanafunzi ambayo hufanyika kila mwisho wa mwenzi wakati wa usiku katika ukumbi wa shule.

Sikukuu hii hutoa fursa ya wanafunzi kuonyesha vipaji vyao mbali mbali.Tukapitia katika cantin ya shule na tukanunua chakula kisha tukaelekea kwenye ukumbi uliojaa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza ahadi cha sita

Shughuli zikaanza huku wanafunzi mbali mbali wakionyesha vipaji vyao huku wakishangiliwa na wanaofanya vibaya huzomewa.Ukumbi ukakaa kimya huku tukiwasubiria washiriki wa shindano la umiss wa shule kupita mbele yetu huku majaji wakiwa ni waalimu wetu wa michezo pamoja na wanafunzi baadhi.

Wakaanza kuingia mmoja mmoja huku wakiwa wamependeza,nikajikuta ninanyanyuka kwa furaha huku nikipiga makofi hii ni baada ya kumuona Salome akiwa katika msururu huo wa mamisi waliochanganyika vidato mbali mbali.

Wakajipanga mbele ya majaji na kuanza kuulizwa maswali mmoja baada ya mwingine kwa lugha ya kingereza.Ikafika zamu ya Salome kuulizwa swali wanafunzi wote wakakaa kimya kumsikiliza atakacho kijibu

“SALOME CAN YOU TELL US WHAT IS LOVE?”(Salome unaweza kutuambia upendo ni nini?)

“Love is force of nature however much we may want to,we can not command,demand or disapper love,any more than we can and in adition love cannot  be bought,sold or trade.You cannot make some one to love you.Thanks”(Upendo ni hali ya msukumo wa kihalisia kwa jinsi tunavyo hitaji.Hatuwezi kulazimisha,kukomalia au kutawanya upendo kwa kadri tunavyoweza na kwa kuongezea Upendo hauwezi kununuliwa kuuzwa au kubadilishana.Hauwezi kumfaya mtu kukupenda wewe.Asante”)

Ukumbi mzima ukapiga makofi kasoro mimi kwani nikajikuta sentensi ya mwisho ya Salome ikijirudia rudia akilini mwangu “YOU CAN CANNOT MAKE SOMEONE TO LOVE YOU”(Huwezi kumfanya mtu kukupenda).Wakatoka ukumbini kwa wimbo walio ingilia kupisha mambo mengine kuendelea huku tukisubiri matokeo kutoka kwa majaji wetu.

Muda wa matokea ukawadia huku washiriki waote wakisimama mbele yatu.Jaji mmoja akaanza kutangaza nafasi kuanzia ya tatu na ya pili huku nafasi ya kwanza akimkabidhi mgeni rasmi ambaye ni mmiliki wa shule kuitangaza huku wakiwa wamebakia washiriki wanne.Tukakaa kimya kusubiria ni nani atakaye nyakua taji kwa mwaka huo

“NA MSHINDI WETU NI……………………..SALOME ALEX EDWARD”

Ukumbi mzima ukanyanyuka na kuanza kupiga makofi ikiwemo mimi huku John akinisukuma sukuma kila wakati huku akinionyeshe jinsi Salome alivyopendeza na kuzidi kuvutia kwenye macho ya wengi.Akaanza kuvalishwa vitu wanavyo valishwa mamisi pale wanapashinda huku akikabithiwa uwa kubwa na mgaeni rasmi.

Muongoza shindano MC akamuomba Salome amchague mtu wa kwenda kucheza naye mziki kwa dakika tano.Salome akachukua kipaza sauti na sote tukakaa kimya kumsikiliza ni nani atapata bahati hiyo ya kuitwa mbele ya ukumbi huo.Salome akatizama tizama na macho yake akaelekea sehemu tuliyokaa sisi.Akanyoosha kidole chake watu wote wakaangalia tulipo sisi

“Eddy hichi kidole ni chako”.John alizungumza huku akinisukuma sukuma kwa kutumia bega lake.Nikanyanyuka kidogo ila Salome akatingisha kidole chake kwamba si mimi ni jamaa aliyekaa kiti cha nyuma yetu ambaye ni kaka mkuu wetu.

Jamaa akanyanyuka kwa furaha huku wezake nyuma wakimtuma akamchezee Salome hadi alainike.Mimi na John tukabaki kama watu wasio amini huku mimi roho ikianza kuniuma kupita maelezo na kumfanya John kuachia msunyo mkali adi watu wa pembeni yetu wakamtazama na kuanza kucheka

“Mademu wengine bwana was**e kama nini” John alizungumza huku akiendelea kutoa misunyo.Jamaa kama alivyoagizwa na wezake akawa anazidi kumshika shika Salome mwili wake huku wanafunzi wakishangilia kwa furaha na kuzidi kunifanya niichukie sikukuu hiyo

“John twende zetu tukalale” Tukanyanyuka kwenye viti vyetu kutokana na mlango wa kutokea upo mbele tukalazimika kupita mbele ya ukumbi huku macho yangu yaliyojaa hasira yakimtazama Salome ambaye naye alinitazama kwa sekunde kadhaa kisha akayapeleka macho yake sehemu nyingine.Tukashuka kwenye ngazi za ghorofa lenye ukumbi wa shule.Kabla hatujafika chini mwanafunzi mmoja akatuita.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger