Ndugu waandishi wa habari tulio mbele yenu ni kamati ya mawaziri wa mikopo ya serikali za wanafunzi wa Elimu ya juu nchini Tanzania na wajumbe wa kamati hii ni mawaziri wa mikopo kutoka vyuo na Taasisi za Elimu ya juu zote nchini.Kamati hii inaundwa na mawaziri,Manaibu waziri na makatibu wa wizara ya mikopo kutoka vyuo vyote nchini.
Kamati ya mawaziri ya mikopo ilianzishwa Rasmi mnamo tarehe 11/10/2015 kwa madhumuni na malengo ya kulinda na kutetea pia kusimamia haki na maslahi ya wanafunzi wa Taasisi za elimu ya juu na vyuo vikuu nchini Tanzania.
Ndugu waandishi wa habari wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania wanatarajia kuingia katika kipindi cha mafunzo kwa vitendo kinachotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwenzi huu ambapo wanafunzi wa Elimu ya juu watatakiwa kufika katika vituo vyao vya kazi vilivyo sambaa nchi nzima tarehe 25/07/2016 ili kuendelea kupata mafunzo kwa vitendo huku wakihudumia umma wa watanzania katika kada mbalimbali kama madaktari,waalimu,maafisa ardhi,waandisi na wachumi.
Ndugu waandishi nwa habari kinachosikitisha ni kwamba mpaka sasa hakuna fedha zozote zilizotolewa na BODI YA MIKOPO wala mchakato unaoendelea kupelekea utolewaji wa fedha hizo. licha ya ukweli kwamba Wanafunzi wengi ni wafadhiliwa wa bodi hiyo, hivyo fedha za nauli pamoja na fedha za kujikimu kwa malazi na chakula wawapo katika mafunzo kwa vitendo zinapaswa kutolewa na bodi hiyo ili kufanikisha azma hii njema ya serikali ya kutoa huduma kwa jamii.
Ndugu waandishi wa habari ni ukweli usio kificho kuwa BODI YA MIKOPO kwa kushirikiana na TCU wanazo taarifa kuwa wanafunzi hawa wanapaswa kuondoka vyuoni mapema tarehe 23/07/2016 lakini mpaka hivi sasa hawaoneshi dalili yoyote ama nia ya kutoa fedha hizo kwa muda muafaka huku wakijua fika kuwa mchakato wa utolewaji wa fedha hizo lazima upitie hatua ya wanafunzi kusaini ili kuthibitisha utayali wa kupokea fedha hizo . Mpaka sasa hivi tukiwa tumebakiwa na takribani siku tano kabla ya kufunga chuo hakuna hata karatasi za kusaini zilizotumwa vyuoni ili kukamilisha zoezi hilo.
Ndugu waandishi wa habari licha ya juhudi nzito zilizofanywa na mawaziri wa mikopo kiutoka vyuo mbalimbali tukishirikiana na menejimenti za vyuo kufanya mawasiliano na hata kukutana ana kwa ana na watendaji wa BODI YA MIKOPO, na hata WIZARA YA ELIMU lakini bado mpaka hivi sasa hakuna jibu muafaka linalotolewa ama lililokwisha kutolewa juu ya upatikanaji na utolewaji wa pesa za kujikimu za wanafunzi wa elimu ya juu katika kipindi hiki cha mafunzo kwa vitendo.
Ndugu waandishi wa habari imekuwa ni utamaduni sasa kwa BODI YA MIKOPPO kutotoa fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa Elimu ya juu nchini kwa wakati mpaka pale inapotokea migomo na maandamano ya wanafunzi jambo ambalo ni kinyume cha mkataba tuliosaini baina yetu na BODI YA MIKOPO.
Ndugu waandishi wa habari ikumbukwe wazi kuwa pesa zinazotolewa na BODINYA MIKOPO kwa wanafunzi wa Elimu ya juu si Hisani bali ni mkopo uliochini ya mkataba na mwanafunzi hulazimika kulipa fedha hizo kwa wakati huku kukiwa na riba ya asilimia sita (6%) kwa mwaka ambayo mwnanafunzi hukatwa mara tuu baada ya kuajiriwa.
AZIMA YA KAMATI
Ndugu waandishi wa habari kutokana na hali hii kamati ya mawaziri wa mikopo ya Elimu ya juu nchini Tanzania tunaitaka serikali kupitia wizara ya Elimu,sayansi,tekinolojia na mafunzo ya ufundi iisimamie BODI YA MIKOPO kutekeleza wajibu wake na kutufikishia fedha za kujikimu wakati wa mafunzo kwa vitendo mapema wiki kesho ili mwanafunzi wanaonufaika na bodi hiyo waweze kusafiri kutoka vyuoni mpaka katika vyuo vyao kutekeleza wajibu wao kwa Taifa hili.
Ndugu waandishi wa habari kamati hii inatoa muda wa masaa sabini na mbili (72) kwa BODI YA MIKOPO kufikisha fedha katika vyuo ambavyo mpaka sasa hawajapata fedha ya kujikimu awamu ya nne na pia kamati hii inaitaka BODI YA MIKOPO kutoa fedha za kujikimu wakati wa mafunzo kwa vitendo ndani ya muda huo.
Ndugu waandishi wa habari kama BODI YA MIKOPO ikishindwa kutekeleza wajibu wake ndani ya masaa sabini na mbili (72) tuliyoyatoa kamati ya mawaziri wa mikopo tutakuwa tayali kuchukua hatua yeyote dhidi ya BODI YA MIKOPO na tutajitokeza mbele ya vyombo vya habari siku ya Jumatano kutangaza kwa umma hatua tutakayoadhimia kuichukua.
IMETOLEWA; TAREHE 16/07/2016
SHITINDI VENANCE MWENYEKITI KAMATI TAIFA.
0759704444
NTILE JOEL
KATIBU KAMATI TAIFA 0754255744
0 comments:
Post a Comment