Sunday 3 July 2016

KANUSHO KUHUSU JOHN MNYIKA KUNENA MAZITO KUHUSU LOWASSA

...

Tokeo la picha la JOHN MNYIKA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAARIFA KWA UMMA
Ipo hoja nyepesi mno iliyopikwa na Vijana wa Lumumba juu ya Mbunge wa Kibamba na Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika kuwa alimkataa Lowassa

Hoja hiyo ni ya kupuuzwa kwa kuwa haina ukweli wowote ule, na nitalishangaa Jeshi la Polisi kuendelea kukaa kimya,na kumuacha aliepotosha Umma kwa kiwango kikubwa kiasi hicho,jambo ambalo limempa Usumbufu mkubwa Naibu Katibu mkuu kwa chama na Wananchi wake katika jimbo lake.

Nataka kuona nguvu ya Cyber Crime kama kweli sheria hiyo ni dhahiri ni msumeno au huwa inakata upande mmoja tu!.Mnyika ni Kiongozi mkubwa na katika Taasisi kubwa sana nchini CHADEMA,hapaswi kunenewa uongo kwa nia ya kuupotosha Umma naliomba jeshi la Polisi liingie kazini Mara moja kutimiza majukumu yake.

Imetolewa July 03

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger