Monday, 3 October 2022

JAMAA AJICHIMBIA KABURI , AWALIPA WATAKAOMLILIA NA ATAYEPIGIA SALUTI MAITI YAKE

...
Mwanaume ambaye amejichimbia kaburi akiwa hai amefunguka kuwa alichukuwa hatua hiyo ili kuwapa watu funzo.


Afrimax iliangazia kwa kina ya mipango madhubiti ya mwanaume huyo ambayo tayari ameweka kwa ajili ya mazishi yake siku za usoni.

Kando na kujichimbia kaburi, tayari amepata watu ambao watamlilia na kumchezea ngoma pamoja na mtu ambaye atapigia saluti maiti yake. Katika mipango yake pia amekamilisha kutayarisha nguo atakazozikwa nazo.

Kulingana na mwanamume huyo, kisa cha kusikitisha cha mwanamume ambaye wanawe wanaishi ng'ambo kilimtia moyo kuwapa watu funzo.

Alijifunza kutoka kwa mtu huyo kwamba watu wanapenda wafu kuliko walio hai. Mzee huyo aliishi katika umaskini wa sina sinani licha ya kuwa na watoto ughaibuni. Alipofariki, wale watoto waliokataa kumtunza akiwa hai, walirudi na kujenga mahali pazuri.

Alipokuwa hai, aliishi katika nyumba iliyobomoka akikabiliwa na njaa huku akivaa nguo chafu. Mtu huyo ambaye jina lake halikutambulika alipanga mazishi akisema anatarajia kuwafunza watu kuwapenda na kuwajali wazazi wao wakati bado wangali hai.

Kama ilivyoripotiwa hapo awali, mwanamume mmoja kutoka Murang'a alianza mipango ya jinsi mazishi yake yatafanywa baada ya kukata roho katika tarehe isiyojulikana. Samuel Karanja, ambaye pia anajiita Kumenya, kumaanisha "Kujua" alijenga eneo lake la kuzikwa ili kuondolea familia yake gharama ya kuchimba kaburi lake atakapokufa.

Akiongea na mwanahabari Victor Kinuthia, mzee huyo alisema pia amejiandika ratiba yake ya mazishi ambayo anatarajia kusomwa wakati wa hafla hiyo kwa sababu hakuna anayemfahamu zaidi yake.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger